Julie Billiart
(Elekezwa kutoka Julia Billiart)
Julie Billiart (Cuvilly, Ufaransa, 12 Julai 1751 — Namur, Ubelgiji, 8 Aprili 1816) alikuwa bikira aliyeanzisha kwa ajili ya malezi ya wasichana shirika la masista wa Bibi Yetu wa Namur mwaka 1803[1].
Alikuwa maarufu kwa upendo wake wa pekee akaeneza kwa bidii ibada kwa Moyo Mtakatifu wa Yesu[2].
Siku hizi masista wake ni 2,000 hivi, nao wanaishi katika nchi 20 za mabara matano, zikiwemo Kenya na Tanzania.
Alitangazwa mwenye heri na Papa Pius X tarehe 13 Mei 1906 halafu mtakatifu na Papa Paulo VI tarehe 22 Juni 1969.
Tazama pia
haririTanbihi
hariri- ↑ http://www.santiebeati.it/dettaglio/48950
- ↑ Online, Catholic. "St. Julie Billiart - Saints & Angels - Catholic Online". www.catholic.org. Iliwekwa mnamo 2016-06-02.
- ↑ Martyrologium Romanum
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |