Papa Pius X (Riese, Veneto, Italia Kaskazini, 2 Juni 1835Roma, 20 Agosti 1914) alikuwa Papa kuanzia tarehe 4/9 Agosti 1903 hadi kifo chake[1]. Alitokea Riese, Treviso, Italia[2].

Mt. Pius X.

Jina lake la kuzaliwa lilikuwa Giuseppe Sarto.

Alimfuata Papa Leo XIII na kuvishwa taji la Kipapa tarehe 9 Agosti 1903, wa kwanza katika karne ya 20. Akafuatwa na Papa Benedikto XV.

Alitangazwa na Papa Pius XII kuwa mwenyeheri tarehe 3 Juni 1951, halafu mtakatifu tarehe 29 Mei 1954.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 21 Agosti[3].

Maisha hariri

Kabla ya kuchaguliwa kama Papa, aliwahi kuwa paroko, askofu wa Mantova (tangu 1884, halafu Patriarki wa Venice (tangu 1893). Hivyo alikuwa na mang'amuzi mengi ya kichungaji.

Kwa kuwa katika uchaguzi makardinali walimpiga kura kwanza mwenzao Rampolla, lakini aliwekewa kura ya turufu na Kaisari wa Austria-Hungaria, mara alipochaguliwa Pius X alifuta haki hiyo ya Kaisari na kuamua atengwe na Kanisa Katoliki yeyote atakayeingilia tena uchaguzi wa Papa.

Lengo lake lilifafanuliwa na kaulimbiu yake: "Instaurare omnia in Christo" Kukamilisha yote ndani ya Kristo.

Kweli alijitahidi kuleta hali mpya katika Kanisa.

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

Viungo vya nje hariri

  Makala hii kuhusu Papa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Papa Pius X kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.