Sesari wa Terracina

(Elekezwa kutoka Juliani na Sesari)

Sesari wa Terracina alikuwa shemasi wa Karthago, leo nchini Tunisia (Afrika Kaskazini) katika karne ya 2.

Padri Juliani na shemasi Sesari wakihubiri.
Shemasi Sesari.

Aliposafiri kwenda Italia, alishuhudia na kupinga ibada ya kuchinja kijana kama kafara kwa mungu Apolo. Kwa ajili hiyo alifungwa miaka miwili na hatimaye akauawa huko Terracina kwa kutoswa baharini ndani ya gunia.

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu mfiadini, pengine pamoja na padri Juliani[1].

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 1 Novemba[2][3].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

Viungo vya nje hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.