Julie Billiart (Cuvilly, Ufaransa, 12 Julai 1751Namur, Ubelgiji, 8 Aprili 1816) alikuwa bikira aliyeanzisha kwa ajili ya malezi ya wasichana shirika la masista wa Bibi Yetu wa Namur mwaka 1803[1].

Mt. Julie Billiart alivyochorwa mwaka 1830.

Alikuwa maarufu kwa upendo wake wa pekee akaeneza kwa bidii ibada kwa Moyo Mtakatifu wa Yesu[2].

Siku hizi masista wake ni 2,000 hivi, nao wanaishi katika nchi 20 za mabara matano, zikiwemo Kenya na Tanzania.

Alitangazwa mwenye heri na Papa Pius X tarehe 13 Mei 1906 halafu mtakatifu na Papa Paulo VI tarehe 22 Juni 1969.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake[3].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.