Goromwe

(Elekezwa kutoka Jumbereru)
Goromwe
Goromwe madoadoa (Synodus variegatus)
Goromwe madoadoa (Synodus variegatus)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Actinopterygii (Samaki walio na mapezi yenye tindi)
Oda: Aulopiformes (Samaki kama goromwe)
Familia: Synodontidae (Samaki walio na mnasaba na goromwe)
Gill, 1862
Ngazi za chini

Jenasi 4 na spishi 79, 19 katika Afrika:

Goromwe au spika ni samaki wa baharini wa familia Synodontidae katika oda Aulopiformes wanaoishi sakafu ya bahari hadi kina cha m 400 katika kanda za tropiki na nusutropiki. Spishi nyingine huitwa bumbo, (m)bumbura au jumbereru.

Maelezo

hariri

Kwa kawaida goromwe ni wadogo, ingawa spishi kubwa zaidi ina urefu wa sm 60. Wana mwili mwembamba wa umbo kama mcheduara na kichwa kinachofanana na kile cha mijusi. Pezimgongo liko katikati ya mgongo na linaongozwa na pezi dogo lenye shahamu karibu na mkia. Wana kinywa kinachojaa na meno makali, hata kwa ulimi.

Ekolojia

hariri

Goromwe ni samaki wa sakafu ya bahari wanaoishi katika maji kame ya pwani; hata spishi za goromwe zinazokaa kwa kina kikubwa huishi katika maji si zaidi ya kina cha m 400. Spishi fulani za jenasi Harpadon huishi katika milango ya mito yenye maji ya chumvi kidogo. Wanapendelea mazingira ya mchanga na huwa na rangi za mwili ambazo zinawasaidia kuwanyerereza katika mazingira kama hayo.

Lava wa goromwe huogelea huria. Wanajulikana kwa uwepo wa mabaka meusi katika matumbo yao yanayoonekana wazi kupitia ngozi yao nyangavu isiyo na magamba.

Spishi za Afrika

hariri

Marejeo

hariri
  • Rashid Anam & Edoardo Mostarda (2012) Field identification guide for the living marine resources of Kenya. FAO, Rome.
  • Gabriella Bianchi (1985) Field guide to the commercial marine brackish-water species of Tanzania. FAO, Rome.

Viungo vya nje

hariri