Goromwe
Goromwe | ||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Goromwe madoadoa (Synodus variegatus)
| ||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||
| ||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||
Jenasi 4 na spishi 79, 19 katika Afrika:
|
Goromwe au spika ni samaki wa baharini wa familia Synodontidae katika oda Aulopiformes wanaoishi sakafu ya bahari hadi kina cha m 400 katika kanda za tropiki na nusutropiki. Spishi nyingine huitwa bumbo, (m)bumbura au jumbereru.
Maelezo
haririKwa kawaida goromwe ni wadogo, ingawa spishi kubwa zaidi ina urefu wa sm 60. Wana mwili mwembamba wa umbo kama mcheduara na kichwa kinachofanana na kile cha mijusi. Pezimgongo liko katikati ya mgongo na linaongozwa na pezi dogo lenye shahamu karibu na mkia. Wana kinywa kinachojaa na meno makali, hata kwa ulimi.
Ekolojia
haririGoromwe ni samaki wa sakafu ya bahari wanaoishi katika maji kame ya pwani; hata spishi za goromwe zinazokaa kwa kina kikubwa huishi katika maji si zaidi ya kina cha m 400. Spishi fulani za jenasi Harpadon huishi katika milango ya mito yenye maji ya chumvi kidogo. Wanapendelea mazingira ya mchanga na huwa na rangi za mwili ambazo zinawasaidia kuwanyerereza katika mazingira kama hayo.
Lava wa goromwe huogelea huria. Wanajulikana kwa uwepo wa mabaka meusi katika matumbo yao yanayoonekana wazi kupitia ngozi yao nyangavu isiyo na magamba.
Spishi za Afrika
hariri- Harpadon nehereus, Bumbura au Jumbereru (Bombay duck)
- Saurida gracilis, Goromwe Mwembamba (Gracile lizardfish)
- Saurida lessepsianus, Goromwe wa Lesseps (Lessepsian lizardfish)
- Saurida longimanus, Goromwe Mapezi-marefu au Semutundu (Longfin lizardfish)
- Saurida macrolepis, Goromwe Magamba-makubwa (Large-scaled lizardfish)
- Saurida tumbil, Goromwe Mkubwa au Bumbo (Greater lizardfish)
- Saurida undosquamis, Goromwe Meno-brashi au Bumbo (Brushtooth lizardfish)
- Synodus binotatus, Goromwe Madoa-mawili (Two-spot lizardfish)
- Synodus dermatogenys, Goromwe-mchanga (Sand lizardfish)
- Synodus indicus, Goromwe Hindi (Indian lizardfish)
- Synodus jaculum, Goromwe Mrukaji (Lighthouse lizardfish)
- Synodus macrops, Goromwe Misalaba-mitatu (Triplecross lizardfish)
- Synodus mascarensis, Goromwe wa Maskarena (Mascarene lizardfish)
- Synodus randalli, Goromwe wa Randall (Randall's lizardfish)
- Synodus saurus, Goromwe wa Atlantiki (Atlantic lizardfish)
- Synodus synodus, Goromwe Almasi (Diamond lizardfish)
- Synodus variegatus, Goromwe Madoadoa (Variegated lizardfish)
- Synodus vityazi, Goromwe wa Madagaska (Synodus vityazi)
- Trachinocephalus myops, Goromwe pua-butu wa Atlantiki (Blunt-nose lizardfish)
- Trachinocephalus trachinus, Goromwe pua-butu wa Indo-Pasifiki (Indo-Pacific blunt-nose lizardfish)
Picha
hariri-
Bumbura
-
Goromwe mwembamba
-
Goromwe magamba-makubwa
-
Goromwe meno-brashi
-
Goromwe madoa-mawili
-
Goromwe-mchanga
-
Goromwe Mrukaji
-
Goromwe misalaba-mitatu
-
Goromwe wa Atlantiki
-
Goromwe Almasi
-
Goromwe pua-butu wa Atlantiki
-
Goromwe pua-butu wa Indo-Pasifiki
Marejeo
hariri- Rashid Anam & Edoardo Mostarda (2012) Field identification guide for the living marine resources of Kenya. FAO, Rome.
- Gabriella Bianchi (1985) Field guide to the commercial marine brackish-water species of Tanzania. FAO, Rome.