Kaliniko na wenzake

Kaliniko na wenzake Imeri, Theodori, Stefano, Petro, Paulo, Theodori, Yohane, Yohane na mwingine asiyejulikana kwa jina (walifia dini karibu na Gaza, Palestina, 638) ni kundi la askari Wakristo waliokamatwa na wavamizi Waislamu lakini, kwa kuhimizwa na askofu Sofroni wa Yerusalemu, walikiri imani yao na kwa ajili hiyo walikatwa vichwa vyao[1].

Tangu kale wanaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama watakatifu wafiadini.

Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 6 Novemba[2].

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.