Khanga
Khanga (au kanga) ni vazi au nguo nyepesi pia ndefu ya rangi ambayo hupendwa kuvaliwa na wanawake, hasa nchi za Afrika Mashariki na Afrika Magharibi. Kanga inafanana na kikoi ambacho kawaida huvaliwa na wanaume.
Kwa kawaida kanga huwa na upana wa sentimita 150 na urefu wa sentimita 110. Kanga huweza kutumiwa kama vazi rasmi, kitambaa cha kichwani, taulo, kitambaa cha mezani na kwa shughuli mbalimbali kama kubeba watoto au kubeba mizigo kichwani.
Hutumiwa pia kama zawadi kwenye sherehe za kuzaliwa, harusi, sikukuku kama vile Eid n.k.[1] Hutolewa pia kwa familia iliyofiwa na ndugu yao nchini Tanzania na hata Kenya.
Mwanzoni kanga ilikuwa ikirembwa kwa vitone vidogo ambavyo vilionekana na manyonya ya ndege aina ya kanga. Ndiyo sababu ilipewa jina hili, kwa sasa Kanga inarembeshwa kwa chapa za maua, majani na hata matunda.
Kanga huwa na sehemu tatu: pindo, mji (sehemu ya kati), na ujumbe. Ujumbe mara nyingi huwa ni kitendawili au fumbo.
Ujumbe huo kwenye kanga hutumika kupitisha ujumbe au fumbo kwa mtu, mfano mke kwa mumewe au swahiba kwa swahibae au kwa swahiba/marafiki, ujumbe unaweza kuwa kwa nia ya kumshukuru, kumkanya, kutoa hongera au kwa ajili ya mapenzi.
Hii ni mifano ya ujumbe wa kwenye kanga.
- Majivuno hayafaif[2]
- Mkipendana mambo huwa sawa
- Japo sipati tamaa sikati [2]
- Wazazi ni dhahabu kuwatunza ni thawabu: [2]
- Sisi sote abiria dereva ni Mungu[2]
- Fimbo la mnyonge halina nguvu[3]
- Mwanamke mazingira tunataka, usawa, amani, maendeleo[2]
- Naogopa simba na meno yake siogopi mtu kwa maneno yake[2].
- Leo ni siku ya shangwe na vigelegele
- Subira huvuta kheri.
- Wawili wakipenda adui hana nafasi.
- Hakuna kama mama.
Marejeo
hariri- ↑ John., Picton, (1995). The art of African textiles : technology, tradition, and lurex. Becker, Rayda., Barbican Art Gallery. London: Barbican Art Gallery. ISBN 0853316821. OCLC 34052769.
{{cite book}}
: CS1 maint: extra punctuation (link) CS1 maint: multiple names: authors list (link) - ↑ 2.0 2.1 2.2 2.3 2.4 2.5 "Alphabetical List of Inscriptions and Their Translations: Kanga & Kitenge: Cloth and Culture in East Africa" (PDF). Erie Art Museum. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 11 Agosti 2012. Iliwekwa mnamo 18 Desemba 2009.
{{cite web}}
: Unknown parameter|deadurl=
ignored (|url-status=
suggested) (help)CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Howden, Daniel (14 Novemba 2009). "Kangalicious: Let your dress do the talking". The Independent. Iliwekwa mnamo 14 Novemba 2009.
Anyone wearing a kanga with the proverb Fimbo La Mnyonge Halina Nguvu" (Might is Right) may know something about the darker side of the garment's journey from the coast into the interior.
{{cite news}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
Viungo vya nje
haririMakala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Khanga kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |