Kanisa kuu la Roma
Kanisa kuu la Roma ni jengo la ibada lililopo tangu karne ya 4 hadi leo katika mtaa wa Laterani mjini Roma.
Ni kwamba, kama majimbo yote ya Kanisa Katoliki, jimbo la Roma, ambalo askofu wake ni mkuu wa maaskofu wote, lina jengo moja la ibada linaloheshimiwa kama ishara ya umoja wa waamini wake.
Likiwa kanisa kuu la Papa, papo hapo ni kanisa kuu la dunia nzima kwa Wakristo wenye ushirika kamili naye.
Kanisa hilo lilijengwa na kaisari Konstantino Mkuu kwa ajili ya maaskofu wa Roma likawekwa wakfu mwaka 314 kwa heshima ya Kristo Mkombozi, lakini linajulikana zaidi kwa jina la Mt. Yohane (Mbatizaji), msimamizi wa Roma.
Sikukuu ya kutabaruku kanisa hilo inaadhimishwa na Wakatoliki wa Kilatini kila mwaka tarehe 9 Novemba[1] kama ishara ya upendo na umoja na Papa [2].
Mitaguso mikuu
haririKatika kanisa hilo mara tano ulifanyika mtaguso mkuu:
wa 9. Mtaguso wa kwanza wa Laterano (1123)
wa 10. Mtaguso wa pili wa Laterano (1139)
wa 11. Mtaguso wa tatu wa Laterano (1179)
wa 12. Mtaguso wa nne wa Laterano (1215)
wa 18. Mtaguso wa tano wa Laterano (1512-1517).
Tanbihi
haririMakala hii kuhusu Kanisa Katoliki bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kanisa kuu la Roma kama historia yake au maelezo zaidi? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |