Karakoram (pia Karakorum) ni eneo la milima mirefu inayopakana na Himalaya upande wa mashariki na Hindu Kush upande wa kusini; eneo hili lipo mpakani mwa Pakistan, Uhindi na China likienea hadi Afghanistan na Tajikistan.

Milima ya Karakoram pamoja na barafuto ya Baltoro; mlima wa Gasherbrum I upande wa kushoto.

Safu za Karakoram zinaenea kwa kilomita 482. Kuna milima mirefu minne yenye kimo juu ya mita 8,000 ambayo ni K2 (m 8.611), Gasherbrum I (m 8.080), Broad Peak (m 8.051) na Gasherbrum II (m 8.035).

Pia kuna barafuto mashuhuri kama vile Siachen na Biafo zinazoenea kwa kilomita 76 na 63.

Sehemu kubwa ya maji kutoka Karakoram huishia katika beseni la mto Indus na kuelekea nao kwenye Bahari Hindi.

Milima mirefu zaidi ya Karakoram hariri

 
K2.

(kimo kwa mita juu ya usawa wa bahari)

Viungo vya nje hariri

 
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Karakoram kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.