Kastulo (alifariki Roma, Italia, 286 hivi) alikuwa Mkristo wa Roma ya Kale aliyeuawa kwa kuzikwa hai wakati wa dhuluma ya kaisari Dioklesyano[1].

Sanamu yake huko Moosburg.

Inasemekana alikuwa na cheo katika ikulu na mume wa Irene wa Roma. Baada ya kuongokea Ukristo alivuta wengi katika dini hiyo[2] na kuficha nyumbani mwake waliotafutwa na serikali kwa ajili ya imani yao[3].

Tangu kale anaheshimiwa na Wakristo wa madhehebu mbalimbali kama mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 26 Machi[4].

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri
  1. http://www.santiebeati.it/dettaglio/47160
  2. "Santos". ACI Prensa. 2007-07-29. Iliwekwa mnamo 2011-06-27.
  3. Ebenezer Cobham Brewer, A Dictionary of Miracles: Imitative, Realistic, and Dogmatic (Chatto and Windus, 1901), 11.
  4. Martyrologium Romanum

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.