Kaunti ya Busia ni mojawapo ya kaunti za Kenya zilizopo baada ya katiba mpya ya Jamhuri ya Kenya kupatikana mwaka 2010.

Ramani ya Busia, Kenya

Wakati wa sensa ya mwaka 2019 wakazi walikuwa 893,681 katika eneo la km2 1,696.3, msongamano ukiwa hivyo wa watu 527 kwa kilometa mraba[1].

Makao makuu yako Busia.

Shughuli kuu ya kiuchumi ni biashara na nchi jirani ya Uganda, pamoja na mji wa Busia kituo cha mpakani.

Mbali na mji, uchumi wa wilaya hutegemea sana uvuvi na kilimo, mazao msingi yakiwa pamoja na mihogo, mtama, viazi vitamu, maharagwe, na mahindi.

Wilaya ya Busia ni makao ya kabila la Waluhya nchini Kenya ambao wanapatikana hasa katika sehemu za Magharibi mwa Kenya.

Utawala

hariri

Kaunti ya Busia ina maeneo bunge saba yafuatayo[2]:

Eeneo bunge Kata
Budalangi Bunyala Central, Bunyala North, Bunyala West, Bunyala South
Butula Marachi West, Kingandole, Marachi Central, Marachi East, Marachi North, Elugulu
Funyula Namboboto, Nambuku Nangina, Bwiri, Ageng'a Nanguba
Matayos Bukhayo West, Mayenje, Matayos South, Busibwabo, Burumba
Nambale Nambale Mjini, Bukhayo North/Waltsi, Bukhayo East, Bukhayo Central
Teso Kaskazini Malaba Central, Malaba North, Ang'urai South, Malaba South, Ang'urai North, Ang'urai East
Teso Kusini Ang'orom, Chakol South, Amukura Central, Chakol North, Amukura East, Amukura West

Idadi ya wakazi katika kaunti ndogo (2019) [3]

hariri
  • Bunyala 85,977
  • Busia 142,408
  • Butula 140,334
  • Nambale 111,636
  • Samia 107,176
  • Teso North 138,034
  • Teso South 168,116

Tazama pia

hariri

Marejeo

hariri
  1. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-11-13. Iliwekwa mnamo 2021-05-30.
  2. http://countytrak.infotrakresearch.com/Busia-county/
  3. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-11-13. Iliwekwa mnamo 2021-05-30.

Viungo vya nje

hariri

0°26′N 34°9′E / 0.433°N 34.150°E / 0.433; 34.150