Wilaya ya Busia, Kenya


Busia ilikuwa wilaya mojawapo ya Mkoa wa Magharibi wa Jamhuri ya Kenya hadi ilipopitishwa katiba mpya ya nchi (2010).

Wilaya ya Busia
Mahali paWilaya ya Busia
Mahali paWilaya ya Busia
Mahali pa Wilaya ya Busia katika Kenya
Nchi Bendera ya Kenya Kenya
Mji mkuu Busia
Eneo
 - Jumla 1,628.4 km²
Idadi ya wakazi (2009 Sensa[1])
 - Wakazi kwa ujumla 743,946

Ilikuwa inapakana na Wilaya ya Kakamega mashariki, Wilaya ya Bungoma kaskazini, Wilaya ya Busia, Uganda upande wa magharibi, na Ziwa Victoria upande wa kusini.

Makao makuu yalikuwa mjini Busia.

Kwa sasa imekuwa kaunti ya Busia.

Shughuli kuu ya kiuchumi ni biashara na nchi jirani ya Uganda, pamoja na mji wa Busia kituo cha mpakani.

Mbali na mji, uchumi wa wilaya hutegemea sana uvuvi na kilimo, mazao msingi yakiwa pamoja na mihogo, mtama, viazi vitamu, maharagwe, na mahindi.

Wilaya ya Busia ni makao ya kabila la Waluhya nchini Kenya ambao wanapatikana hasa katika sehemu za Magharibi mwa Kenya. Wilaya hii ilikuwa na wakazi 370,608 (1999 sensa).

Mamlaka za Mitaa (Halmashauri)
Mamlaka Aina Idadi ya Watu Wakazi wa mjini*
Busia Manispaa 44,766 30,777
Funyula Manispaa 18,043 1,242
Nambale Mji 26,168 1,005
Port Victoria Mji 18,472 5,917
Manispaa ya Busia Manispaa 263,159 5,516
Jumla -- 370,608 44,457
* 1999 census. Source: [1]
Maeneo ya utawala
Tarafa Idadi ya Watu Wakazi wa mjini* Makao makuu
Budalangi 53,356 5,417
Butula 95,489 4,805 Butula
Funyula 73,875 1,106 Funyula
Matayos 56,186 0 Matayos
Nambale 67,544 0 Nambale
Township 25,158 15,695 Busia
Jumla 370,608 27,022 --
* 1999 census. Sources: [2], [3],

Wilaya ya Busia ina maeneo bunge manne:

Tazama pia

hariri

Marejeo

hariri

Viungo vya nje

hariri

0°26′N 34°9′E / 0.433°N 34.150°E / 0.433; 34.150