Kaunti ya Mandera ni mojawapo ya kaunti za Kenya zilizopo baada ya katiba mpya ya Jamhuri ya Kenya kupatikana mwaka 2010. Imepakana na Kaunti ya Wajir, na nchi za Somalia na Uhabeshi.

Kaunti ya Mandera
Kaunti
Nembo ya Serikali
Mandera County in Kenya.svg
Kaunti ya Mandera katika Kenya
Coordinates: 3°25′00″N 40°40′00″E / 3.41667°N 40.6667°E / 3.41667; 40.6667
Nchi Kenya
Namba9
IlianzishwaTarehe 4 Machi, 2013
Ilitanguliwa naMkoa wa Kaskazini Mashariki
Makao MakuuMandera
Miji mingineEl Wak
GavanaAli Ibrahim Roba
Naibu wa GavanaArai Mohamed Ahmed
SenetaMohamed Maalim Mahamud
Mbunge Mwanamke(Bunge la Taifa)Amina Gedow Hassan
Bunge la KauntiBunge la Kaunti ya Mandera
Wawakilishi wa Bunge la Kaunti waliochaguliwa30
Maeneo bunge/Kaunti ndogo6
Eneokm2 25 939.8 (sq mi 10 015.4)
Idadi ya watu867,457
Wiani wa idadi ya watu33
Kanda mudaSaa za Afrika Mashariki (UTC+3)
Tovutimandera.go.ke

Wakati wa sensa ya mwaka 2019 wakazi walikuwa 867,457 katika eneo la km2 25,939.8, msongamano ukiwa hivyo wa watu 33 kwa kilometa mraba[1]..

Makao makuu yako Mandera.

Jiografia hariri

Kaunti hii ina mbuga ya pekee ya Kaskazini Mashariki ya Malka Mari na hifadhi ya kibinafsi ya Chacnabole[2]. Ina vilima vinavyo tandaa kutoka El Wak hadi Uhabeshi ingawa kiasi kikubwa cha ardhi yake ni nchi tambarare. Kuna kanda mbili za ikolojia, kavu na nusu kavu. 95% ya kaunti ni nusu kavu na huwa na vichaka vyenye miiba katika sehemu za chini za vilima[3].

Utawala hariri

Kaunti ya Mandera imegawanywa katika maeneo yafuatayo[4]:

Eneo Bunge/Kaunti ndogo Kata
Mandera West Takaba Kusini, Takaba, Lagsure, Dandu, Gither
Banissa Banissa, Derkhale, Guba, Malkamari, Kiliwehiri
Mandera North Ashabito, Guticha, Marothile, Rhamu, Rhamu Dimtu
Mandera South Wargadou, Kutulo, Elwak Kusini, Elwak Kaskazini, Shimbir Fatuma
Mandera East Arabia, Libehia, Khalalio, Neboi, Mandera Mjini
Lafey Sala, Fino, Lafey, Waranqara, Alango Gof

Idadi ya wakazi katika kaunti ndogo (2019) [5] hariri

  • Mandera West 98,300
  • Banisa 152,598
  • Kutulo 72,394
  • Lafey 83,457
  • Mandera Central 157,220
  • Mandera East 159,638
  • Mandera North 143,850

Tazama pia hariri

Marejeo hariri

  1. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-11-13. Iliwekwa mnamo 2021-05-29. 
  2. "Mandera County", E-Limu, ilipatikana 13-04-2018
  3. "KENYA INTER AGENCY RAPID ASSESSMENT MANDERA COUNTY CONFLICT ASSESSMENT REPORT 19TH – 30TH JUNE 2014", Kenya Inter Agency Assessment, ilipatikana 13-04-2018
  4. "Kaunti ya Mandera", Infotrak, ilipatikana 13-04-2018
  5. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-11-13. Iliwekwa mnamo 2021-05-29. 

Viungo vya nje hariri