Khalila Mbowe

Mnenguaji wa Kitanzania, mbunifu wa uongozaji filamu na mjasiriamali wa jamii

Khalila Kellz Mbowe ni msanii kutoka nchini Tanzania, mwanzilishi na afisa mtendaji mkuu wa Unleashed African Company Limited (UACL), taasisi inayofundisha vijana wenye vipaji husika katika sanaa za jukwaani na kuwashauri katika matumizi ya sanaa hizo. [1] [2]

Khalila Kellz Mbowe
Nchi Tanzania
Kazi yake mkoreographia

Alizaliwa Tanzania mnamo mwaka 1988, [2] akasoma "Saint Mary’s Secondary School" jijini Dar es Salaam kwa masomo yake ya shule ya upili. Akaendelea kusoma Chuo Kikuu cha Taylor, huko Singapuri hadi kupata cheti katika fani ya Mawasiliano mnamo 2010.

Kwa sasa amejiunga na masomo ya biashara kwa njia ya intaneti kwenye Chuo Kikuu cha Watu, [3] kilichopo Marekani.

Mnamo 2006, akiwa na umri wa miaka 18, alipata ajira yake ya kwanza kwenye kampuni ya matangazo ya FCB iliyo sehemu ya Lowe Scanad Tanzania Limited [2].

Mwaka 2008 alikuwa na akiba ya kutosha ili aweze kusoma Singapuri.

Mnamo mwaka 2010, baada ya kuhitimu kutoka [Chuo kikuu]] cha Taylor, alipata kazi kwa Airtel Tanzania alipokaa kwa mwaka mmoja, kuanzia 2013 hadi 2014. Kuanzia Aprili 2015 hadi Desemba 2015, alifanya kazi kama afisa mtendaji wa "Buddies Production Company Limited", kampuni ya televisheni kutoka Uganda ambayo ilikuwa ikitaka kupanuka Tanzania. [2]

Tangu Februari 2015, amejikita katika kuendesha kampuni yake ya UACL akifuata pia masomo yake ya biashara kupitia intaneti. Kampuni yake iliajiri watu 20 kuanzia Novemba 2017. Wateja wake wengine wamejumuisha Vodacom, Total Tanzania, Taasisi ya Uongozi, TED Global na Sera Project. [2]

Familia

hariri

Khalila Mbowe ni mama wa watoto wawili; Raphael, amezaliwa mnamo 2009 na Belle, alizaliwa karibu 2014. [2]

Marejeo

hariri
  1. SE Forum (2015). "About Khalila and Unleashed". Social Entrepreneurship Forum (SE Forum). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-11-14. Iliwekwa mnamo 14 Novemba 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. 2.0 2.1 2.2 2.3 2.4 2.5 Uliwa, Caroline (11 Novemba 2017). "Khalila Mbowe: A go-getter from an early age". Iliwekwa mnamo 14 Novemba 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. Pappano, Laura (1 Novemba 2013). "The Value in a Free Degree: Where Are the Graduates of University of the People?". Iliwekwa mnamo 14 Novemba 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Khalila Mbowe kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.