Kigamboni ni kata ya wilaya ya Kigamboni iliyo na postikodi namba 17107.

Feri ya Kigamboni mjini Dar es Salaam
Mapumziko Kigamboni ufukoni

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 24,810 [1]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 30,496 waishio humo.[2]

Kigamboni ina umbo la rasi kati ya Bahari Hindi na maji ya bandari. Imetengwa na jiji la Dar es Salaam kwa maji ya Kurasini Creek.

Mawasiliano yapo kwa njia ya feri kati ya Kigamboni na Kivukoni upande wa jiji.

Kiasili sehemu hii ilikuwa kijiji cha wavuvi lakini katika miaka ya nyuma watu wa jijini wamejenga nyumba na hoteli za kitalii zimeenea kwenye ufuko wa Bahari Hindi.

Marejeo

hariri
  Kata za Wilaya ya Kigamboni - Tanzania  

Kibada (17109) | Kigamboni (17107) | Kimbiji (17101) | Kisarawe II (17104) | Mjimwema (17106) | Pembamnazi (17105) | Somangila (17102) | Tungi (17103) | Vijibweni (17108)