Kikatalunya

(Elekezwa kutoka Kikatalonia)

Kikatalunya au kikatalani (kwa Kikatalunya: català) ni mojawapo kati ya lugha za Kirumi ambayo ni lugha rasmi ya jimbo la Katalunya, Valencia na visiwa vya Baleari katika ufalme wa Hispania (Ulaya kusini magharibi) na vilevile utemi wa Andorra. Pia inatumika katika sehemu za Ufaransa kusini na Italia visiwani.

Wanaoitumia kama lugha ya kwanza ni watu milioni 4.1 na kama lugha ya pili ni milioni 5.1.

Historia ya lugha

hariri

Asili ya lugha hiyo ni katika nchi ya Hispania, na lugha iliyoizaa ni Kilatini cha Waroma wa Kale waliotawala kwa muda mrefu Hispania.

  Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kikatalunya kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.