Korčula (tamka kor-chu-la) ni kisiwa cha Kroatia katika Bahari ya Adria na pia jina la mji mdogo uliopo mle.

Mji wa Korcula.

Kisiwa cha Korcula huwa na eneo la km2 278; urefu wake ni km 46.8 na upana wake ni km 7.8 km kwa wastani [1]. Kipo karibu sana na pwani. Idadi ya wakazi wa kisiwa ni watu 15,522 (2011).

Jina la kisiwa lilitokana na walowezi Wagiriki waliofika katika karne ya 6 KK kutoka kisiwa cha Korfu (kwa Kigir.: Korkira, Κόρκυρα)[2]. Waliita makazi yao mapya Melaina Korkira (Μέλαινα Κόρκυρα) yaani Korkira Nyeusi, kutokana na misitu minene waliyoikuta kisiwani. Tangu mwaka 220 KK kisiwa, pamoja na pwani yote ya Dalmatia, kilikuwa sehemu ya Dola la Roma.

Katika karne ya 6 na 7 BK makabila ya Waslavi (mababu ya Wakroatia wa leo) yalifika kwenye pwani ya Dalmatia[3] .

Wakati wa karne za kati utawala wa Korcula ulibadilika kati ya Venisi, Hungaria, Kroatia na Serbia pamoja na vipindi vya kujitawala kabisa. Tangu karne ya 15 ilikuwa tena chini ya Venisi hadi kuwa sehemu ya Milki ya Austria kwenye mwaka 1815 hadi kuwa sehemu ya Yugoslavia mnamo 1918 baada ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia. Tangu kuporomoka kwa umoja wa Yugoslavia mwaka 1991 imekuwa mji wa Kroatia.

Siku hizi Korcula ina uchumi unaotegemea utalii.

Marejeo hariri

  1. Duplančić Leder, Tea; Ujević, Tin; Čala, Mendi (June 2004). "Coastline lengths and areas of islands in the Croatian part of the Adriatic Sea determined from the topographic maps at the scale of 1 : 25 000". Geoadria (Zadar) 9 (1): 5–32. doi:10.15291/geoadria.127. Iliwekwa mnamo 1 December 2019.  Unknown parameter |doi-access= ignored (help); Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
  2. An Inventory of Archaic and Classical Poleis: An Investigation Conducted by The Copenhagen Polis Centre for the Danish National Research Foundation by Mogens Herman Hansen, 2005, Index
  3. A History of the Croatian by Francis Ralph Preveden (1955)