Kunguni-maji mtambaazi

(Elekezwa kutoka Kumguni-maji mtambaazi)
Kunguni-maji mtambaazi
Ilyocoris cimicoides
Ilyocoris cimicoides
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Arthropoda (Wanyama wenye mwili wa pingili na miguu ya kuunga wasio na ugwe wa mgongo kama wadudu, nge, buibui)
Nusufaila: Hexapoda (Arithropodi wenye miguu sita)
(bila tabaka): Dicondylia (Wadudu walio na mandibula zenye condyle mbili)
Ngeli: Insecta (Wadudu)
Nusungeli: Pterygota (Wadudu wenye mabawa)
Oda ya juu: Paraneoptera
Oda: Hemiptera
Haeckel, 1896
Nusuoda: Heteroptera
Oda ya chini: Nepomorpha
Familia ya juu: Naucoroidea
Familia: Naucoridae
Leach, 1815
Ngazi za chini

Nusufamilia 5; jenasi 46, 6 katika Afrika ya Mashariki:

Kunguni-maji watambaazi ni wadudu wadogo wa majini wa familia Naucoridae katika oda ya chini Nepomorpha ya oda Hemiptera walio na miguu ya mbele yenye femuri pana sana. Wanafanana na kunguni-maji wakubwa lakini spishi zote ni ndogo. Kuna spishi takriban 400 katika jenasi 46. Jenasi 6 zinapatikana Afrika ya Mashariki[1].

Maelezo

hariri

Kunguni-maji watambaazi wana urefu wa sm 0.5-2. Mwili wao ni bapa na una umbo la duaradufu. Miguu yao ya mbele ina femuri pana na imara sana zenye takriban umbo la pembetatu inayotumiwa kukamata mbuawa. Miguu ya nyuma haikutoholewa sana kwa kuogelea, kwa sababu huogelea kwa nadra bali hutambaa zaidi kwenye sakafu. Sehemu za kinywa ni imara na kama sindano. Kwa kawaida wadudu hao wana mabawa yaliyokuzwa vizuri.

Biolojia

hariri

Wadudu hao huwa wanakaa kwenye sakafu ya maji au kati ya mimea ambapo hutafuta mbuawa. Wanatokea katika maji, yanayotiririka au la, yenye oksijeni nyingi, hivyo wanaweza kukaa chini ya maji kwa muda mrefu kabla ya kwenda usoni ili kubadilisha hewa ya plastron yao kubwa (eneo la mwili lenye vinywele vingi vinashikilia hewa) chini ya mabawa. Mbuawa anapokaribia wanamshika kwa miguu yao imara ya mbele. Kisha wanamtoboa kwa kinywa chao na kuingiza mate ambayo hufanya tishu kuwa kiowevu. Baada ya hayo wanafyonza yaliyomo. Mbuawa ni pamoja na konokono, gegereka wadogo (viroboto wa maji, amfipoda na isopoda), wadudu wadogo na lava wao.

Kama kunguni wakubwa wa maji kunguni hao wanaweza kuuma vidole vya mikono vya watu, lakini hiyo inatukia kwa kawaida wakishikwa tu. Inaonekana kwamba umo lao linauma zaidi.

Majike hutaga mayai yao kati ya mimea au changarawe. Wanaweza kuruka vizuri lakini hawaonekani mara nyingi wakiruka.

Spishi za Afrika ya Mashariki

hariri
  • Aneurocoris insolitus
  • Ctenipocoris africanus
  • Laccocoris limicola
  • Laccocoris limigenus
  • Laccocoris spurcus
  • Macrocoris convexus
  • Macrocoris flavicollis
  • Macrocoris laticollis
  • Afronaucoris kenyalis
  • Afronaucoris obscuratus
  • Neomacrocoris bondelaufa
  • Neomacrocoris handlirschi
  • Neomacrocoris karimii
  • Neomacrocoris ndugai
  • Neomacrocoris parviceps
  • Neomacrocoris schaeferi
  • Neomacrocoris usambaricus
  • Neomacrocoris vuga

Marejeo

hariri
  1. Sites, Robert W. (7 Februari 2022). "Phylogeny and revised classification of the saucer bugs (Hemiptera: Nepomorpha: Naucoridae)". Zoological Journal of the Linnean Society: 1–42. doi:10.1093/zoolinnean/zlab105.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)