Loje ni kata ya Wilaya ya Chamwino katika Mkoa wa Dodoma, Tanzania, yenye postikodi namba 41432[1]. Imepakana na kata ya Chipogoro (wilaya ya Mpwapwa) upande wa mashariki ambapo barabara ya kati ya Afrika inapita.

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 7,916 [2]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 5,134 [3] waishio humo.

Loje ina mchanganyiko wa makabila ambayo hupatikana humo kama vile Wagogo (wenyeji), Wasukuma, Wamasai na makabila mengine ya Tanzania kulingana na mwingiliano wa shuguli za uvuvi kando ya bwawa la Mtera, lakini lugha inayotawala ni Kigogo.

Shughuli za kiuchumi ambazo ni za uhakika na fursa kwa wakazi kuongeza kipato chao ni kilimo cha mazao (mtama, mahindi, viazi vitamu, ufuta), ufugaji (ng'ombe, mbuzi, kondoo, kuku, nguruwe), uvuvi (kambi za Igunguli, Uwanja wa Ndege), ujasiriamali mdogo.

Marejeo

hariri
  1. "Nakala iliyohifadhiwa" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2020-03-21. Iliwekwa mnamo 2017-10-08.
  2. https://www.nbs.go.tz
  3. "Sensa ya 2012, Dodoma - Chamwino DC" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2004-01-02. Iliwekwa mnamo 2016-05-18.
  Kata za Wilaya ya Chamwino - Mkoa wa Dodoma - Tanzania  

Buigiri | Chamwino mjini | Chiboli | Chilonwa | Chinugulu | Dabalo | Fufu | Handali | Haneti | Huzi | Idifu | Igandu | Ikombolinga | Ikowa | Iringa Mvumi | Itiso | Loje | Majeleko | Makang'wa | Manchali | Manda | Manzase | Membe | Mlowa Barabarani | Mlowa Bwawani | Mpwayungu | Msamalo | Msanga | Muungano | Mvumi Makulu | Mvumi Misheni | Nghahelezi | Nghambaku | Nhinhi | Segala | Zajilwa


  Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Dodoma bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Loje kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.