Mahmoud Ahmed Abdulkadir
Mahmoud Ahmed Abdulkadir (amejulikana zaidi kwa jina la Ustadh Mau;alizaliwa tarehe 20 Februari 1952 – ).Ustadh Mau ni mshairi na imamu kutoka kisiwa cha Lamu, Kenya. Mashairi na hotuba zake zinahusu jamii, umuhimu wa elimu, huruma na wajibu wa kijamii.
Mahmoud Ahmed Abdulkadir | |
Nchi | Kenya |
---|---|
Majina mengine | Ustadh Mau |
Kazi yake | mshairi na imamu |
Maisha
haririUstadh Mau kamwe hakuhudhuria shule ya serikali; elimu yake yote ya Kiswahili na ya Kiarabu alipata kwa walimu wa Kiislamu katika madrasa na vyuo vya Kiislamu vya eneo hilo.
Tangu mwaka 1985, amekuwa imamu wa Msikiti wa Pwani, msikiti wa zamani zaidi Lamu. Alikuwa imamu wa kwanza Lamu kutoa hotuba zake za Ijumaa kwa lugha ya Kiswahili. Ustadh Mau alisimamia bakershop ya familia hadi mwaka 2005. [1]
Maktaba
haririUstadh Mau ni mpenda vitabu. Maktaba yake binafsi inakusanya mashairi ya Kiswahili yaloandikwa kwa herufu za ajami, na vijitabu na kumbukumbu kutoka Mashariki ya Kati na India. Karibu tungo na hotuba elfu mbili kutoka kwenye maktaba yake binafsi kwa sasa vinapigwa picha na kuhifadhiwa Maktaba ya Makavazi ya Lamu kwa msaada wa ruzuku ya MEAP [2] (kwa hati zilizoandikwa na rekodi za sauti zilizonakiliwa tazama Ustadh Mau Digital Archive). [3]
Marejeo
hariri- ↑ Kresse, K., & Swaleh, K. (2022). "Ustadh Mahmoud Mau, Mtu wa watu (“A Man of the People”): Poet, Imam, and Engaged Local Intellectual". In: In This Fragile World. Leiden, The Netherlands: Brill. (Online hapa)
- ↑ Modern Endangerd Archives Program (MEAP)
- ↑ Raia, A. (2022). "Seeking ʿilm on Lamu: Ustadh Mau’s Library and Services for the Benefit of His Community". In In This Fragile World. Leiden, The Netherlands: Brill. (Online hapa)
Vyanzo
hariri- In this fragile world : Swahili poetry of commitment by Ustadh Mahmoud Mau / Poetry by Ustadh Mau (Mahmoud Ahmed Abdulkadir). Translated and edited by Annachiara Raia and Clarissa Vierke, in collaboration with Jasmin Mahazi and Azra Ahmad Abdulkadir. Leiden ; Boston : Brill, [2023] (Online version)
- Mahmoud Ahmed Abdulkadir (mau): Mshairi mcheza kwao lakini asiyetuzwa / Rayya Timammy. In: Lugha na fasihi katika karne ya Ishirini na Moja. Kwa heshima ya marehemu Profesa Naomi Luchera Shitemi, edited by Mosol Kandagor, Nathan Ogechi, and Clarissa Vierke, Eldoret: Moi University Press, 2017, pages 231–242.
- Shaykh Mahmoud Abdulkadir "Mau" : a reformist preacher in Lamu / Rayya Timammy. In: Annual Review of Islam in Africa, 2014, vol. 12., no. 2, pages 85-90.
Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mahmoud Ahmed Abdulkadir kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |