Karibu kwenye Wikipedia kwa Kiswahili!

Twamfurahia kila mmoja anayeingia na kuungana nasi. Hii ni kamusi elezo ya maandishi huru. Unaweza kuandika makala uipendayo - hata kuitafsiri kutoka katika Wikipedia kwa lugha nyingine. Kwa mawili matatu labda tazama:

Jisikie huru kuuliza swali lolote lihusianalo na Wikipedia hii. Karibu kujitambulisha kwenye "Ukurasa wa mtumiaji". Ukitaka kupata kwanza uzoefu wa kuweza kuhariri Wikipedia, tafadhali tumia ukurasa wako kwa majaribio. Humo unaruhusiwa kujipatia uzoefu wa uundaji wa makala za Wikipedia! Juu yako mwenyewe uandike pekee kwenye ukurasa wako wa mtumiaji. Humo uko huru kutangaza chochote upendacho, kama si biashara au matusi.

Ujue miiko:

Tunakushauri pia kuandikisha email yako; haitaonekana na wengine lakini wataweza kukuandikia kupitia mfumo wa Wikipedia. Karibu sana!


Welcome to Kiswahili Wikipedia!

We welcome you even if you don't speak Kiswahili. For a bot flag go to this site. If you try to edit entries as a non-speaker, it is better to first communicate with one of our admins who can advise you. You may find them at Wikipedia:Wakabidhi. And, please:

  • do not post computer translated texts (like Google Translate, Content Translation, etc. all do not work for Swahili)
  • nor copied texts/images from other webs to this site!
  • do not use links to commercial pages, never post anything that looks like advertising.

As a newcomer we advise that you register your email. This will not be visible to others but it allows us to notify you, which often is helpful in case of problems.

Kipala (majadiliano) 10:29, 14 Novemba 2017 (UTC)

Halafu naomba ukumbuke kupanga makala katika jamii na kuiunganisha na lugha nyingine (interwiki). Kipala (majadiliano) 10:29, 14 Novemba 2017 (UTC)

Nimeona mara nyingi anaandika makala kweli bila jamii. Lakini tumpe muda atazoea. Akiwa na tabia ya kupitia makala alizoanzisha, itamsaidia kuona wapi alipotoka!--MwanaharakatiLonga 09:31, 7 Desemba 2017 (UTC)

MawasilianoEdit

Hreflafa tunafurahi ya kwamba umejiunga na wikipedia hii na kuchangia. Lakini naona pia ya kamba hujaanza kuwasiliana na kujibu ukipata habari. Hii si vizuri, msingi mmoja muhimu wa kazi yetu ni kuwasiliana na kushauriana. Jinsi unavyokaa kimyakimya hatuwezi kujua kama labda hujaelewa utaratibu, unaogopa kujibu au unapuuza ushauri. Kwa hiyo sisi wengine tuko hapa kwa lengo la kukusaidia. Hapo chini naongeza jambo niliyoona katika makala yako ya maabara. Kipala (majadiliano) 08:37, 26 Aprili 2018 (UTC)

Kuhusu maabara na kuchunguza madaEdit

Ukichangia ni muhimu kufanya uchunguzi kwanza. Siku hizi ni afadhali kuongeza pia ushahidi (ingawa idadi kubwa ya makala bado hakuna). Katika mfano wa maabara ulijaribu kutafsiri matini kutoka enwiki. Kwa bahati mbaya matini hii si nzuri sana na hivyo umechanganya mambo kidogo. Wakieleza matumizi ya neno "laboratory" katika lugha ya Kiingereza wewe uliona hii inahusu historia ya maabara katika nchi ya Uingereza. Ukifanya utafiti kidogo utaelewa ni nini maana ya neno hili "alchemy" wanayotumia (alkemia - makala hii hatujaanza bado). Kwa utafiti kidogo ungeelewa pia maana ya "Big Science". Kwa hiyo si vema kutafsiri matini kutoka enwiki bila kuchungulia na kuelewa vema. Jinsi ilivyo historia hii sasa inatupe picha ya kwamba maabara yalibadilika hasa kwa ajili ya kuunda "zana za vita za kiatomiki" tena katika Uingereza na hii yote si sahihi.

Usikate tamaa kama nyongeza hizi hazibaki, ni kawaida hii ni njia jinsi gani wikipedia inakua na kuboreshwa. Lakini fanya utafiti. Sisi tuko tayari kukushauri namna gani. Uliza tu usiogope. Kipala (majadiliano) 09:04, 26 Aprili 2018 (UTC)

Kwa KipalaEdit

Ni mambo mengi sana sielewi. Haswa likija swala la majadiliano. Sijui hata kama nafanya vizuri saa hii nikihariri hapa. Kwanza nimeona kuwa nikiandika makala mapya, kuna wengine wanaongeza jamii ya makala hayo. Ningependa kujua jinsi ya kuongeza jamii hizo. Pili, ni vipi, majina yenu yanavyokuwa na rangi ya buluu. Ningependa kujua na kuonyeshwa nanyi [Hreflafa]

Naona umeleta makala ya mauzo dijitali. Maombi 2: 1) usisahau kuipanga katika Jamii. Hapa unatafakari kwanza inaingia jamii gani (hii: labda Jamii:Biashara). 2) uiwekee katika Interwiki yaani kuiunganisha na makala mengine kuhusu maada hii kwa lugha tofauti (kama yapo). Hapa unapeleleza kwanza ni makala gani inayolingana kwa Kiingereza (labda ulitumia makala ya Kiingereza na kutafsiri sehemu zake?). Halafu angalia upande wa kushoto chini kwenye desktop utaona "Lugha" na "Add links". Bofya Add links halafu unapata madirisha mawili; juu andika enwiki na thibitisha "English (enwiki)", chini yake andika jina la makala ya Kiingereza halafu thibitisha. Ukiwa na swali, uniulize. Kipala (majadiliano) 08:33, 10 Septemba 2018 (UTC)

Kwa Kipala Asante sana kwa kunielekeza katika hili. Nitalifuata na nikiwa na tatizo nitaomba msaada

sawa, andika chini ya matini yote [[Jamii:Biashara]] - hapa usitumie visual editor. Ukijibu tia sahihi hapa ukurasa wa majadiliano (si katika makala!) kwa kutumia alama hizi mwishoni ~~~~ Kipala (majadiliano) 08:49, 10 Septemba 2018 (UTC)

Asante. Nimelifanya hilo na ikaweka Jamii Biashara pale chini Hreflafa (majadiliano) 09:15, 10 Septemba 2018 (UTC)

Vizuri, hongera! Sasa tafuta makala ya Kiingereza inayolingana (je iko? labda digital marketing? Kama ni hii weka pia Kiingereza chake kwa mabano na italiki baada ya lemma ya Kiswahili. Kipala (majadiliano) 21:54, 10 Septemba 2018 (UTC))

Hili la kuunganisha makala ya Kiswahili bado sijalielewa. Huenda kukawa na makala yanayoeleza jambo hili niyatumie. AsanteHreflafa (majadiliano) 09:56, 13 Septemba 2018 (UTC)

Je umejaribu kufuata hatua zilizopo juu? Interwiki ni orodha ya lugha unayooana upande wa kuchoti chini kwa makala mengi. Ili zionekane lazima kuziunganisha na database kuu ya Wikidata. Basi fuata hatua nilizoandika. au soma hapa https://en.wikipedia.org/wiki/Help:Interwiki_linking#Interlanguage_linksKipala (majadiliano) 20:59, 13 Septemba 2018 (UTC)
Halafu naomba tuachane na mizaha. Ulileta hizi makala kuhusu Hofu ya Jumapili na CBD Gummies. Nimepeleka yote miwili kwenye mapendekezo ya Wikipedia:Makala kwa ufutaji. Unaweza kuzitetea huko ukipenda. Kipala (majadiliano) 20:59, 13 Septemba 2018 (UTC)

Maandishi ya hofu ya Jumapili (Sunday Scaries) ni jambo lililo na umaarufu. Mengi yameandikwa kuhusu hisia hii katika wavuti kama Forbes, NBC news, thisisinsider, businessinsider na Thrive Global yote ambayo ni majalada yenye umaarufu. Hreflafa (majadiliano) 11:15, 14 Septemba 2018 (UTC)

Makala haina chanzo kimoja kinachoeleza hali hii ni nini. Nikipitilia "google" napata maelezo tofauti sana. Inaonekana ni kitu kinachojadiliwa katika tovuto huko Marekani, lakini hii haiundi bado jambo. Karibu kuitetea kwenye ukurasa wa makala za ufutaji. Kipala (majadiliano) 13:14, 14 Septemba 2018 (UTC)

Hongera kwa kuboresha makala hadi hapa. Lakini bado vyanzo. Ukihitaji msaada, uliza. Ona kwanza viungo vilivyotajwa katika boksi ya "Makala haina vyanzo vya kutosha" niliyoweka pale (baada ya kurejibisha itafutwa tena). Nadhani unaweza kuchukua marejeo kutoka enwiki, nisipokosei Kipala (majadiliano) 09:26, 22 Septemba 2018 (UTC)

Tovuti za biasharaEdit

Naona karibu kila mara unaweza viungo vya tovuti za biashara, kitu ambacho hakitakiwi. Kwa kweli mara nyingine nashawishika kufikiri kwamba lengo lako ni kuwafanya wasomaji wetu wanunue kitu. Wikipedia si mahali pa mauzo dijitali! Amani kwako. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 08:53, 28 Septemba 2018 (UTC)

Leo nakuonya mara ya mwisho. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 10:52, 1 Machi 2019 (UTC)
Nd Hreflava ni vizuri ukitafuta kwenye intaneti tovuti ambazo zina mifano na maelezo zaidi kuhusu kichwa cha makala. Ila si kila tovuti inayofaa. Hasa haifai kuleta hapa kurasa za makampuni yanayouza vifaa. Nakubali ya kwamba wakati mwingine wana picha bora na wakati mwingine pia maelezo mazuri. Lakini zinafaa mara chache tu. Heri hadi uongeze uzoefu jaribu sasa kwa nusu mwaka kutotumia kabisa tovuti za makampuni kwa marejeo (isipokuwa ukiona kuna kampuni muhimu, hapa tunaunganisha na tovutiy a wenyewe - lakini kama makala ni kuhusu kampuni hii, si kuhusu vifaa).Kipala (majadiliano) 14:24, 1 Machi 2019 (UTC)