Karibu kwenye Wikipedia kwa Kiswahili!

Tunamfurahia kila mmoja anayeingia na kuungana nasi. Hii ni kamusi elezo ya maandishi huru. Unaweza kuandika makala uipendayo ama kuitafsiri kutoka Wikipedia ya lugha nyingine.

Ukipenda kutumia kurasa zetu za mwongozo na msaada, a) ukitumia simu bofya kwa "Dawati" chini kwenye dirisha lako na b) ubadilishe mwonekano wa Wikipedia kwa kubofya "Switch to old look" kwenye menyu upande wa kushoto.

Kwa mawili matatu labda tazama:

Jisikie huru kuuliza swali lolote lihusianalo na Wikipedia hii. Karibu kujitambulisha kwenye "Ukurasa wa mtumiaji". Ukitaka kupata kwanza uzoefu wa kuweza kuhariri Wikipedia, tafadhali tumia ukurasa wako kwa majaribio. Humo unaruhusiwa kujipatia uzoefu wa uundaji wa makala za Wikipedia! Juu yako mwenyewe uandike tu kwenye ukurasa wako wa mtumiaji. Humo uko huru kutangaza chochote upendacho, kama si biashara au matusi.

Ujue miiko:

  • usilete kamwe matini wala picha kutoka tovuti za nje.
  • usiingize matangazo ya kibiashara (pamoja na kuelekeza kwa kurasa zenye matangazo).
  • usimwage kamwe matini kutoka google-translate au programu za kutafsiri.
  • usitumie kama vyanzo vya taarifa au tanbihi <ref>Wikipedia (au mradi mwingine wa Wikimedia)</ref>, ila unaweza kutumia vyanzo vyake kwa kuvitaja vyenyewe moja kwa moja.

Tunakushauri pia kuandikisha email yako; haitaonekana na wengine lakini wataweza kukuandikia kupitia mfumo wa Wikipedia. Karibu sana!


Welcome to Kiswahili Wikipedia!

We welcome you even if you don't speak Kiswahili. For a bot flag go to this site. If you try to edit entries as a non-speaker, it is better to first communicate with one of our admins who can advise you. You may find them at Wikipedia:Wakabidhi. And, please:

  • do not post computer translated texts (like Google Translate, Content Translation, etc. all do not work for Swahili)
  • nor copied texts/images from other webs to this site!
  • do not use links to commercial pages, never post anything that looks like advertising.
  • do not use as references <ref>Wikipedia (or another project of Wikimedia)</ref>, though you can use their references by writing them themselves.

As a newcomer we advise that you register your email. This will not be visible to others but it allows us to notify you, which often is helpful in case of problems.

Czeus25 Masele (majadiliano) 09:31, 17 Septemba 2020 (UTC)Reply

Wachagga

hariri

Habari zako, naona nyongeza yako ndefu kuhusu Wachagga / maoni kuhusu Wachagga. Kwa bahati mbaya hujaonyesha chanzo chochote. Matini yako inaonekana kama maoni matupu. Ingekuwa vizuri pale facebook au jamii forums lakini haileti elimu. Ukiwa na ushahidi Wachagga husafiri kushinda watu wengine - basi lete na uandike. Kama una ushahidi watu wanauliza sana kwa nini Wachagga wanasafiri - basi ulete ushahidi. Menginevyo napendekeza kifungu kifutwe. Kipala (majadiliano) nina ushahidi kaka sababu mimi mwenyewe natoka huko. ukitaka kuamini wachaga wanaongoza kwa kwenda desemba angalia hali ya usafiri kipindi hicho kutoka Dar kwenda Moshi Kilimanjaro mpaka gari ndogo huwa zinaenda.

sikaelewa kwenye kuweka link kama ushahidi kwa chapisho langu. vipi ikiwa ni habari mpya? au nimejazia habari? je ni makala zote zina ushahidi? kama mwandishi ndio mtu wa kwanza ataweka ushahidi wa link kutoka wapi?

Habari ndugu Kibosho Singa (majadiliano) 13:12, 16 Januari 2021 (UTC)Reply

Kwema Kibosho Singa (majadiliano) 10:12, 29 Mei 2021 (UTC)Reply

Ndugu, ukisikitika kwamba lugha yetu haijasonga mbele zaidi, njoo kutuunga mkono katika Wikipedia yetu kama ulivyofanya kuhusu Taliban. Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 08:29, 20 Agosti 2021 (UTC)Reply

Asante ndugu yangu, nitajitahidi japo bado nina ugeni na mambo mengi sana. Kibosho Singa (majadiliano) 10:41, 20 Agosti 2021 (UTC)Reply

Picha

hariri

Jamani nawezaje kujifunza jinsi ya kuweka picha kwenye jukwaa? Natanguliza shukrani kwa wote Kibosho Singa (majadiliano) 07:30, 26 Agosti 2021 (UTC)Reply

Sijui unasema jukwaa gani. Ukipenda kuweka picha katika makala, njia nzuri ni kunakili kutoka lugha nyingine na kutafsiri sehemu ya mwisho tu. Kwa mfano: [[File:Fgvby.jpg.|thumb|This is John.]] kufanya: [[File:Fgvby.jpg.|thumb|Huyu ni John.]]. Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 11:26, 26 Agosti 2021 (UTC)Reply

Asante ndugu yangu,kwa hiyo wewe kama wewe huwezi kupqkia picha katika habari yako? Kibosho Singa (majadiliano) 11:42, 26 Agosti 2021 (UTC)Reply

Kama ni hivi, soma Msaada:Picha. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 11:52, 26 Agosti 2021 (UTC)Reply

Asante kaka nimeelewa Kibosho Singa (majadiliano) 13:54, 26 Agosti 2021 (UTC)Reply

Muundo wa Makala

hariri

Habari ndugu,

Pongezi kwa jitahada zako za uchangiaji, tafadhali wakati unapokua unaazisha makala jitahidi kuzingatia vigezo vyote vinavyohitajika kwenye makala kuwa bora na yenye tija, pitia ukurasa huu "Msaada wa kuanzisha makala" kujifunza zaidi namna ya kuaziasha makala kwa ufasaha, mfano wa makala uliyoanzisha hii "Young Killer Msodokiu" imekosa sifa za kimuundo pamoja na vyanzo.

Nyongeza kwenye hilo pia jaribu kuwa unapitia makala ulioanzisha nyuma mara kwa mara ili kuona wahariri wengine wamechangia nini kwenye makala hiyo ili kuandelea kujifunza zaidi.

Amani kwako Anuary Rajabu (majadiliano) 19:46, 4 Mei 2023 (UTC)Reply

sawa mkuu nimekupata Kibosho Singa (majadiliano) 07:18, 5 Mei 2023 (UTC)Reply