We' bwana, salaam! Unashauri wende polepole kidogo angalau upate msaada kutoka kwa wachangiaji wenzako!

Karibu kwenye Wikipedia kwa Kiswahili!

Tunamfurahia kila mmoja anayeingia na kuungana nasi. Hii ni kamusi elezo ya maandishi huru. Unaweza kuandika makala uipendayo ama kuitafsiri kutoka Wikipedia ya lugha nyingine.

Ukipenda kutumia kurasa zetu za mwongozo na msaada, a) ukitumia simu bofya kwa "Dawati" chini kwenye dirisha lako na n) ubadilishe mwonekano wa Wikipedia kwa kubofya "Switch to old look" kwenye menyu upande wa kushoto.

Kwa mawili matatu labda tazama:

Jisikie huru kuuliza swali lolote lihusianalo na Wikipedia hii. Karibu kujitambulisha kwenye "Ukurasa wa mtumiaji". Ukitaka kupata kwanza uzoefu wa kuweza kuhariri Wikipedia, tafadhali tumia ukurasa wako kwa majaribio. Humo unaruhusiwa kujipatia uzoefu wa uundaji wa makala za Wikipedia! Juu yako mwenyewe uandike tu kwenye ukurasa wako wa mtumiaji. Humo uko huru kutangaza chochote upendacho, kama si biashara au matusi.

Ujue miiko:

Tunakushauri pia kuandikisha email yako; haitaonekana na wengine lakini wataweza kukuandikia kupitia mfumo wa Wikipedia. Karibu sana!


Welcome to Kiswahili Wikipedia!

We welcome you even if you don't speak Kiswahili. For a bot flag go to this site. If you try to edit entries as a non-speaker, it is better to first communicate with one of our admins who can advise you. You may find them at Wikipedia:Wakabidhi. And, please:

  • do not post computer translated texts (like Google Translate, Content Translation, etc. all do not work for Swahili)
  • nor copied texts/images from other webs to this site!
  • do not use links to commercial pages, never post anything that looks like advertising.

As a newcomer we advise that you register your email. This will not be visible to others but it allows us to notify you, which often is helpful in case of problems.

--Muddyb Mwanaharakati Longa 07:12, 21 Juni 2021 (UTC) Reply

Ndugu, asante na pongezi kwa kutunga makala nyingi, ila kabla hujaendelea soma vizuri maelekezo ya hapa juu. Kwanza kabisa usikubali tafsiri ya kompyuta bila kuipitia kwa makini ili kuhakikisha inaeleweka kweli. Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 06:20, 25 Juni 2021 (UTC)Reply

Vyanzo hariri

Salamu, pitia katika makala zako za mwisho uone namna gani ya kuweka vyanzo, vyanzo vinavyotokana na makala za Wikipedia ya Kiingereza havikubaliki katika wikipedia ya Kiswahili, na unapoanza kuhariri makala yako hakikisha haufuti vyanzo vilivyopo katika makala ya kiingereza,pia ni vyema ukapitia makala kadhaa ambazo zimekwisha andikwa tayari ili kuona namna uhariri unavyofanyika,Amani sana Idd ninga (majadiliano)

Nimekuzuia kwa kumwaga google translate hariri

Taarifa ya kukuzuia!

Ndugu, imenibidi kukuzuia kwa sababu zinazotajwa chini. Wakati unapokuwa umezuiwa huwezi kuhariri isipokuwa penye huu ukurasa wako wa majadiliano. Unaweza kunijibu kwa kutumia “Email this user”.

Sababu ni kuwa umeingiza matini iliyopatikana kwa njia ya tafsiri ya kompyuta ikiwa na kasoro nzito ya lugha. Umearifiwa kwamba ni marufuku kumwaga matokeo ya google translate katika makala zetu. Wachangiaji wanaopuuza utaratibu huu wanasababisha hasara kubwa kwa Wikipedia yetu na kuwapa wengine kazi kubwa mno ya kusafisha makosa yao.

Bila shaka una nia nzuri kuchangia katika Wikipedia. Tutafurahi kushirikiana nawe lakini ni lazima ufuate utaratibu. Kazi yetu kama wakabidhi ni kulinda mradi huu.

Ukiwa tayari kufuata utaratibu pamoja na kupitia upya matini ulizozileta tayari, naomba uwasiliane nami kwa kufungua ukurasa wangu (bofya jina langu chini) na kuniandikia baruapepe kwa kubofya “Email this user” upande wa kushoto. Hapo nitaweza kukuruhusu tena. Hapo lazima uwezeshe njia kwa kufuata maelezo katika Wikipedia:Email.

Kipala (majadiliano) 08:50, 12 Agosti 2021 (UTC) Reply


Ndugu, nipo tayari kwa kufanya malekebisho ili niweze kuendelea kutoa mchango wangu katika wikipedia, Naomba unifungulie MR MANAGER123 (majadiliano) 08:56, 5 Oktoba 2021 (UTC)Reply
Ndugu ninakupa sasa nafasi ya kusahihisha makala hizo mbili: Nozipho Bhengu, VVU / UKIMWI nchini Jamaika. Unahitaji kutumia lugha inayoeleweka, kutumia vyanzo vinavyokubaliwa, na kama unategemea kutafsiri, lazima usitafsiri neno-kwa-neno lakini ueleze yale yaliyo ya maana kwa Kiswahili kizuri. Unaweza kufupisha habari ya enwiki lakini unapaswa kuchagua sehemu ya habari ambayo inaleta maana. -- Baada ya kurekebisha niandikie email (tumia "Email this user") kwenye ukurasa wangu na usiendelee hadi tumewasiliana tena. Kipala (majadiliano) 10:36, 5 Oktoba 2021 (UTC)Reply
HABARI, nimejaribu kufanya mabadiliko kwenye makala mbili ambazo nilikosea Nozipho Bhengu, VVU / UKIMWI nchini Jamaika. MR MANAGER123 (majadiliano) 12:54, 20 Novemba 2021 (UTC)Reply

Napaswa kukuonya tena! ona Soufiane El Bakkali, umeweka bila kujali fomati (herufi koze mwanzoni), jamii, viungo vya ndani. tafadhali urekebishe mara moja. Kipala (majadiliano) 09:33, 3 Desemba 2021 (UTC)Reply

Ona Gleb Bakshi. hii afadhali, hata hapa umepuuza fomati, jamii, halafu matumizi yako ya herufi kubwa ni hovyo ("Mwalimu wa Michezo Anayeheshimiwa)". Kipala (majadiliano) 09:35, 3 Desemba 2021 (UTC)Reply
sawa naomba niweze kupitia mapungufu ayo MR MANAGER123 (majadiliano) 21:07, 6 Desemba 2021 (UTC)Reply
Asante kwa kujaribu masahihishao. Sasa ukutunga makala kuhusu wanamichezo, uweke pia jamii inayolingana na riadha, mfano. Ikiwezekana kufuatana na nchi. Kipala (majadiliano) 08:10, 14 Desemba 2021 (UTC)Reply

Viungo hariri

Tafadhali, uunganishe makala zako na interwiki (lugha nyingine) pembeni. Asante na amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 09:02, 8 Machi 2022 (UTC)Reply

Vyanzo vya Kiingereza hariri

Salamu Ndugu, hongera kwa kuendelea na uhariri katika Wikipedia ya Kiswahili, napenda kukutaarifu kuwa link za Wikipedia ya Kiingereza hazifai kutumika kama marejeo katika Wikipedia ya Kiswahili, Amani Sana Idd ninga (majadiliano) 09:39, 11 Aprili 2022 (UTC)Reply

Sawa nitalifayia kazi ilo asante kwa taarifa MR MANAGER123 (majadiliano) 13:53, 13 Aprili 2022 (UTC)Reply

Jamii hariri

Ndugu, naona maendeleo yako. Hata hivyo, unapoweka chini jamii, zisiwe pana mno: kwa mfano mchezaji unampanga katika jamii:Michezo. Kumbe kuna jamii:Wachezaji wa mpira wa kikapu na nyingine za namna hiyo. Naomba urekebishe mwenyewe makala zako mpya. Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 12:21, 2 Septemba 2022 (UTC)Reply

nashukuru nitajitaidi kurekebisha makosa MR MANAGER123 (majadiliano) 17:59, 2 Septemba 2022 (UTC)Reply