Shadrack Masaga
Karibu kwenye Wikipedia kwa Kiswahili!
Tunamfurahia kila mmoja anayeingia na kuungana nasi. Hii ni kamusi elezo ya maandishi huru. Unaweza kuandika makala uipendayo ama kuitafsiri kutoka Wikipedia ya lugha nyingine.
Ukipenda kutumia kurasa zetu za mwongozo na msaada, a) ukitumia simu bofya kwa "Dawati" chini kwenye dirisha lako na b) ubadilishe mwonekano wa Wikipedia kwa kubofya "Switch to old look" kwenye menyu upande wa kushoto.
Kwa mawili matatu labda tazama:
- Kuhusu ukurasa wako wa mtumiaji na kurasa nyingine
- Ukurasa wa mwongozo
- Jamii:Msaada (makala zilizomo humo zinaweza kusaidia mara nyingi)
- Ukurasa wa jumuia (pamoja na Wikipedia:Wakabidhi, penye majina walio tayari kukusaidia)
- Makala za msingi za Wikipedia
Jisikie huru kuuliza swali lolote lihusianalo na Wikipedia hii. Karibu kujitambulisha kwenye "Ukurasa wa mtumiaji". Ukitaka kupata kwanza uzoefu wa kuweza kuhariri Wikipedia, tafadhali tumia ukurasa wako kwa majaribio. Humo unaruhusiwa kujipatia uzoefu wa uundaji wa makala za Wikipedia! Juu yako mwenyewe uandike tu kwenye ukurasa wako wa mtumiaji. Humo uko huru kutangaza chochote upendacho, kama si biashara au matusi.
Ujue miiko:
- usilete kamwe matini wala picha kutoka tovuti za nje.
- usiingize matangazo ya kibiashara (pamoja na kuelekeza kwa kurasa zenye matangazo).
- usimwage kamwe matini kutoka google-translate au programu za kutafsiri.
- usitumie kama vyanzo vya taarifa au tanbihi <ref>Wikipedia (au mradi mwingine wa Wikimedia)</ref>, ila unaweza kutumia vyanzo vyake kwa kuvitaja vyenyewe moja kwa moja.
Tunakushauri pia kuandikisha email yako; haitaonekana na wengine lakini wataweza kukuandikia kupitia mfumo wa Wikipedia. Karibu sana!
Welcome to Kiswahili Wikipedia!
We welcome you even if you don't speak Kiswahili. For a bot flag go to this site. If you try to edit entries as a non-speaker, it is better to first communicate with one of our admins who can advise you. You may find them at Wikipedia:Wakabidhi. And, please:
- do not post computer translated texts (like Google Translate, Content Translation, etc. all do not work for Swahili)
- nor copied texts/images from other webs to this site!
- do not use links to commercial pages, never post anything that looks like advertising.
- do not use as references <ref>Wikipedia (or another project of Wikimedia)</ref>, though you can use their references by writing them themselves.
As a newcomer we advise that you register your email. This will not be visible to others but it allows us to notify you, which often is helpful in case of problems.
--CGN2010 (majadiliano) 19:54, 9 Septemba 2010 (UTC)
Salam, mimi ni mhandisi ya Köln (Cologne=CGN), Ujerumani. Lakini nasema Kiswhahili kidogo tu. Unasema Kiingereza? Tazama Wikipedia:Babel. CGN2010 (majadiliano) 19:25, 11 Septemba 2010 (UTC)
- Ndio nasema kiingereza na kiswahili.--Shadrack Masaga (majadiliano) 16:08, 18 Septemba 2010 (UTC)
Salaam Ndugu Shadrack, nimefurahi sana upanuzi wako wa makala ya Bumbuli. Nilipoanzisha makala mbegu za kata za Tanzania ilikuwa ndoto yangu ya kwamba wenyeji wa sehemu fulani watakuja na kuongeza ujuzi wao. Asante sana! Kuhusu vipengele vya makala nitaandika palepale lakini hii ni hatua ya pili au tatu. Je, umeweka makala zako katika orodha yako ya "maanaglizi yangu"? Kipala (majadiliano) 15:13, 12 Septemba 2010 (UTC)
- Hey, see Kigezo:User ksb. You can put it on top of Mtumiaji:Shadracknaftal like this (if you speak ksb):
{{Babel|ksb|sw|en-1|user-tz}}
Best, --CGN2010 (majadiliano) 21:44, 14 Septemba 2010 (UTC)
- Bwana Shadrack, salaam! Kuna makala kadhaa kama wachawi na Mbegha yaliyoanzishwa na mtumiaji asiyejiandikisha. Nikiona viungo vyao nafikiri labda wewe umeandika.
- Ninaleta ombi lifuatalo: a) ombi ni ukumbuke kujiandikisha (ingawa wakati mwingine tunasahau hata mimi) maana kama kuna maswali au hoja juu ya makala inasaidia mawasiliano. b) usishtuke ukiulizwa juu ya makala maana kuwasiliana hivi ni kawaida yetu. Kamusi hii inajengwa kwa ushirikiano. c) hali halisi kuna maswali juu ya makala hizi mbili: kuhusu mbegha mtumiaji mwingine alikuta habari ambazo ni tofauti kwa hiyo inahitaji mawasiliano kama mnajadili jambo lilelile. Kuhusu wachawi kuna tayari makala uchawi je kuna kitu cha kuunganisha au tufute tena? Kipala (majadiliano) 10:04, 16 Septemba 2010 (UTC)
Ni mimi niliyeandika kuhusu uchawi na nilikuwa sijaelewa vizuri kwani mara ya kwanza niliendeleza maana ya uchawi na baadae niliona neno wachawi limewekewa alama nyekundu ndiyo nikaliandika maelezo ya kuliendeleza. Sasa makala ni lile lile. Sasa inaweza kufutwa moja ile ya wachawi ikabaki ya uchawi au yoyote kati ya hizo ifutwe tu.
Salaam, Shadrack Masaga! Makakala husika na hicho kichwa hapo juu si mbaya, ila tu utaratibu wa kamusi elezo ni kwamba inapendelea sana kutaja umri wa muhusika mwanzo kabla ya mengine. Si lazima sana, lakini idadi kubwa ya makala za kamusi elezo zinakuwa namna hiyo. Kingine jamii, jamii ni nguzo thabiti ya kutambua makala zilizoandikwa kwenye wikipedia. Ndiyo maana unaona kila makala mwisho inakuwa na jamii. Jamii ni kama ifutavyo, sharti ujue unachokiandika kina chimbuko gani na itakuwa rahisi kutaja jamii. Kwa mfano huyu sista ni mtu wa wapi? Ikiwa ni Mwitalia, basi jamii yake ni: jamii:Watu wa Italia ikiwa sambamba na jamii:Watu wa Tanzania kwa sababu kambi yake ipo Tanzania! Pia, unaweza kuongeza kitu kama hiki. Mengineyo utaratibu tutaelekezana.--MwanaharakatiLonga 07:42, 20 Septemba 2010 (UTC)
Mayo
haririSallam ND Shadrack, umepanusha makala Mayo, asante. Nimepeleka masahihisho madogo. Kwa vichwa vidogo ndani ya makala tunatumia njia jinsi unavyoweza kuona hapa: Wikipedia:Mwongozo_(Muundo)#Vichwa na vichwa vidogo. Karibu kujenga kamusi yetu, karibu kuuliza swali lolote! Kipala (majadiliano) 19:52, 21 Septemba 2010 (UTC)
Mponde
haririSalaam, nafurahi jinsi unavyoendelea kupanusha makala za kata za Usambaani. Kuhusu vichwa vidogo vya ndani kuna njia nyepesi ya kupata umbo linalolingana na kawaida yetu (ingawa inachukua muda kidogo kuizoea..). Tazama Wikipedia:Mwongozo_(Muundo)#Vichwa na vichwa vidogo hapa kuna maelezo yote. Upande wa "unaandika" utaona jinsi ya kuandika kwenye dirisha la kuhariri, upande wa "unapata" ni matokeo. Faida yake ni hasa kama makala inakua zaidia na vichwa vidogo vya ndani vinaongezeka basi wikipedia inaingiza orodha ya yaliyomo kwa makala hii. Tena iansaidia kuwa na muundo 1 kwa makala zote inamsaidia msomaji asiyehitaji kuzea uso mpya kila makala. Karibu kujaribu mwenyewe! Kipala (majadiliano) 07:18, 28 Septemba 2010 (UTC)
Kura ya kuamua juu ya wakabidhi waliopotea
haririKaribu kutembelea ukurasa wa wakabidhi na kuamua juu ya wenzetu waliopewa haki za wakabidhi lakini hawakuonekana tangu miezi mingi: Wikipedia:Wakabidhi#Kura_ya_kuondoa_wakabidhi_waliopotea. Tuliwahi kujadili swali hili mwaka uliopita (tazama kwenye ukurasa unaotajwa, juu ya pendekezo) ; sasa njia imeonekana. Kipala (majadiliano) 05:27, 1 Oktoba 2010 (UTC)