Makari wa Aleksandria
Makari wa Aleksandria (300 hivi - 395)[1] alikuwa mmonaki maarufu katika jangwa la Nitria.
Alikuwa kijana zaidi kidogo kuliko Makari Mkuu, ndiyo sababu anaitwa pengine Makari Kijana.[2]
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki, Waorthodoksi na Waorthodoksi wa Mashariki kama mtakatifu.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 19 Januari[3] au 1 Mei.
Maisha
haririMzaliwa wa Aleksandria, alikuwa mfanyabiashara hadi umri wa miaka 40, alipobatizwa na kwenda kuishi jangwani.
Baada ya miaka kadhaa, alipewa upadrisho na kufanywa priori wa monasteri fulani, katika mlima Nitria.[4]
Mwaka 335, Makari alikwenda kuishi peke yake katika jangwa la el-Natroun[2] akiwa mkuu wa wakaapweke zaidi ya elfu tano.
Miujiza mingi inasimuliwa kuwa ilifanywa kwa maombezi yake.
Alipofikia umri wa miaka 73 Makari alipelekwa uhamishoni na Kaisari Valens, pamoja na Makari Mkuu wakaishi katika kisiwa fulani ambacho walifaulu kukiinjilisha.
Tazama pia
haririTanbihi
hariri- ↑ Lives of Saints :: Bashons 6
- ↑ 2.0 2.1 "St. Macarius of Alexandria". www.stabanoub-dallas.org (kwa Kiingereza (Uingereza)). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-03-17. Iliwekwa mnamo 2018-03-17.
- ↑ Martyrologium Romanum
- ↑ http://www.stjohndc.org/Russian/saints/SaintsE/e_0207_Macarius.htm Ilihifadhiwa 7 Julai 2013 kwenye Wayback Machine. "St. Macarius of Alexandria", St. John's Orthodox Church
Marejeo kwa Kiswahili
hariri- Misemo ya Mababa wa Jangwani (Apophthegmata Patrum) – tafsiri ya W. Ngowi, O.F.M.Cap. – ed. Salvatorianum – Morogoro 2000 – ISBN 0-264-66350-0
Viungo vya nje
hariri- Healy, Patrick. "Macarius." The Catholic Encyclopedia. Vol. 16 (Index). New York: The Encyclopedia Press, 1914
- Butler, Alban. The Lives of the Saints, Volume I, 1866
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |