Musoma (mji)
Musoma ni mji wa Tanzania uliopo kwenye mwambao wa mashariki wa Ziwa Viktoria. Musoma imepata halmashauri na hadhi ya manisipaa. Manispaa hiyo inapakana na Wilaya ya Musoma Vijijini.
Musoma | |
Mahali pa mji wa Musoma katika Tanzania |
|
Majiranukta: 1°29′24″S 33°48′0″E / 1.49000°S 33.80000°E | |
Nchi | Tanzania |
---|---|
Mkoa | Mara |
Wilaya | Musoma Mjini |
Idadi ya wakazi | |
- Wakazi kwa ujumla | 108 242 |
Msimbo wa posta | 31101 - 31113 |
Ni makao makuu ya Mkoa wa Mara.
Katika sensa ya mwaka 2002, idadi ya wakazi wa mji huo ilihesabiwa kuwa 108,242 [1].

Historia Edit
Kabla ya ukoloni eneo la Musoma lilikuwa nchi ya Wakabwa, kundi la Wajaluo waliowahi kuhamia hapa.[2]
Wajerumani wa kwanza walifika mnamo mwaka 1910: walikuwa wamisionari, kwa majina Dominik na Paulo, waliojenga makazi na shule karibu na makao ya Mtemi Nyabange[3].
Wakafuatwa na afisa wa kwanza Mjerumani aliyeitwa na wenyeji "Bwana Sirusi" mwenye kazi ya afisa forodha. Huyu Sirusi alihamia mahali pa Musoma ya leo kwa sababu huko kina cha maji ufukoni kilifaa zaidi kwa meli kufika[4]. Hivyo Musoma ilianzishwa kama bandari na baadaye makao ya ofisa mdogo wa Mkoa wa kikoloni wa Mwanza.
Baada ya kuondolewa kwa Wajerumani, Waingereza waliingia. Katika eneo la kudhaminiwa la Tanganyika Musoma ilikuwa makao makuu ya wilaya (district) ikaingia vile katika Tanzania huru.
Mwalimu Julius Nyerere alisoma shule hapa Musoma kuanzia mwaka 1934 na tarehe 21 Januari 1953 alirudi hapa kufunga ndoa na Maria Waningu Gabriel Magige katika Kanisa Katoliki la Musoma Mwisenge [5].
Marejeo Edit
Viungo vya Nje Edit
Kata za Manisipaa ya Musoma - Mkoa wa Mara - Tanzania | ||
---|---|---|
Buhare | Bweri | Iringo | Kamunyonge | Kigera | Kitaji | Makoko | Mukendo | Mwigobero | Mwisenge | Nyakato | Nyamatare | Nyasho |
Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Mara bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Musoma (mji) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. Usiingize majina ya viongozi au maafisa wa sasa maana wanabadilika haraka mno. |