Maria Alfonsina Danil

Maria Alfonsina Danil (Yerusalemu, Palestina, 4 Oktoba 1843Ein Karem, Palestina, 25 Machi 1927) alikuwa mtawa wa Palestina, mwanzilishi wa shirika la Masista Wadominiko wa Rozari Takatifu wa Yerusalemu[1].

Picha yake.

Maisha yake yote alihudumia mafukara wa nchi yake. Kabla ya kuanzisha shirika lake mwaka 1880, alikuwa sista wa lingine, lakini alieleza kuwa njozi za Bikira Maria alizojaliwa akiwa Bethlehemu zimemuelekeza kuanzisha jipya[2].

Papa Benedikto XVI alimtangaza mwenye heri tarehe 22 Novemba 2009[3], halafu Papa Fransisko akamtangaza mtakatifu tarehe 17 Mei 2015[4].

Sikukuu yake huadhimishwa kila mwaka tarehe 25 Mei[5].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  1. Baunard, Louis (1892). Histoire de la vénérable mère Madeleine-Sophie Barat : fondatrice de la Société du Sacré-Cur de Jésus. Paris: Ch. Poussielgue. 
  2. "Beatification soon for Mother Marie-Alphonsine?", Latin Patriarchate of Jerusalem. Retrieved on 2020-05-17. Archived from the original on 2016-03-04. 
  3. "New energy for Mideast with Beatification of native", 25 November 2009. Retrieved on 29 November 2009. Archived from the original on 8 June 2011. 
  4. "The Pope Canonizes Four New Saints", Diocese of Orlando. Jalada kutoka ya awali juu ya 2021-01-16. Iliwekwa mnamo 2020-05-17.
  5. Martyrologium Romanum

Viungo vya nje hariri

 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.