Margerita wa Youville

(Elekezwa kutoka Maria Margareta wa Youville)

Margerita wa Youville (kwa Kifaransa Marie-Marguerite Dufrost de Lajemmerais d'Youville; Varennes, Quebec, 15 Oktoba 1701Montreal, Quebec, 23 Desemba 1771) alikuwa mwanamke Mkristo wa Kanada ambaye, baada ya kufiwa mumewe, alielekeza wanae wawili kwenye upadri akajitosa kwa nguvu zake zote kuhudumia wagonjwa, wazee na wenye shida za kila aina, akaanzisha shirika la kitawa la Masista wa Upendo wa Montreal [1].

Marguerite d'Youville alivyochorwa na James Duncan.

Papa Yohane XXIII alimtangaza mwenye heri mwaka 1959, na Papa Yohane Paulo II mtakatifu tarehe 9 Desemba 1990, akiwa wa kwanza mzaliwa wa Kanada[2].

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake[3] au 16 Oktoba.

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.