Maria wa Kleopa (kwa Kigiriki Μαρία ἡ τοῦ Κλωπᾶ, María hē tou Clōpá) alikuwa mwanamke Myahudi aliyemfuata Yesu Kristo hadi msalabani huko Kalivari (Yoh 19:25)[1].

Huzuni ya Maria wa Kleopa kadiri ya mchoro wa Caravaggio Mazishi ya Kristo (1602).

Haieleweki vizuri kama alikuwa binti au mke wa huyo Kleopa. Wengine wanadhani ndiye aliyetajwa kati ya wanawake waliokwenda kaburini Jumapili asubuhi na mapema kadiri ya Mk 16:1 kama Maria wa Yakobo (bin Alfayo) kwa maana ya mama yake[2].

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu, hasa tarehe 24 Aprili[3].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  1. http://www.santiebeati.it/dettaglio/49100
  2. S. S. Smalley, Dean Emeritus of Chester Cathedral, England. "Mary," New Bible Dictionary, 1982 p. 793.
  3. Martyrologium Romanum
  Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Maria wa Kleopa kama habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.