Mariano, Yakobo na wenzao

Mariano, Yakobo na wenzao Sekondiani, Konkordi, Marinus, Heliodori, Saturnini, Silvani na wengineo wengi (walifia dini Lambesa, leo nchini Algeria, 259) walikuwa Wakristo waliouawa kwa upanga kwa ajili ya imani yao wakati wa dhuluma ya kaisari Valeriani.

Mariano alikuwa msomaji aliyekwishapitia kishujaa dhuluma ya kaisari Decius kwa kuungama imani yake. Katika hiyo mpya alikamatwa pamoja na rafiki yake Yakobo shemasi na baada ya kuvumilia mateso mengi ya kikatili huku wakifarijiwa na Mungu, waliuawa pamoja na wenzao [1].

Tangu kale wanaheshimiwa kama watakatifu wafiadini.

Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 6 Mei[2][3].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  1. https://catholicsaints.info/saint-james-of-numidia/
  2. Martyrologium Romanum: ex Decreto Sacrosancti oecumenici Concilii Vaticani II instauratum auctoritate Ioannis Pauli P.P. II promulgatum, Romae 2001, ISBN 8820972107
  3. http://catholicsaints.info/butlers-lives-of-the-saints-saints-james-marian-and-companions-martyrs-in-numidia/
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.