Polandi
Polandi (kwa Kipolandi: Polska) ni nchi ya Ulaya ya Kati. Imepakana na Ujerumani upande wa magharibi, Ucheki na Slovakia upande wa kusini, Ukraini na Belarusi upande wa mashariki na Bahari ya Baltiki, Lituanya na Urusi (mkoa wa Kaliningrad Oblast) upande wa kaskazini.
| |||||
Kaulimbiu ya taifa: Hakuna | |||||
Wimbo wa taifa: Kipolandi: Mazurek Dąbrowskiego (Mazurka ya "Dąbrowski") | |||||
Mji mkuu | Warshawa | ||||
Mji mkubwa nchini | Warshawa | ||||
Lugha rasmi | Kipolandi[3] | ||||
Serikali | Jamhuri Andrzej Duda Donald Tusk | ||||
Chanzo cha taifa Kupokea Ukristo[4] |
966 | ||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
312,696[1][2] km² (ya 70) 3.07% | ||||
Idadi ya watu - 30 Juni 2014 kadirio - Msongamano wa watu |
38,483,957 (ya 34) 123/km² (ya 83) | ||||
Fedha | Złoty (tamka: swoti) (PLN )
| ||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
CET (UTC+1) CEST (UTC+2) | ||||
Intaneti TLD | .pl (pia .eu kama sehemu ya Umoja wa Ulaya) | ||||
Kodi ya simu | +48
| ||||
1Kibelarusi, Kikashubi, Kijerumani and Kiukraini zinatumiwa kieneo lakini si lugha rasmi za kitaifa.
2 |
Jiografia
haririArdhi ya Polandi ni tupu tu kufikia kiasi cha Bahari ya Baltiki katika upande wa kaskazini mwa Milima ya Carpathi kusini mwa nchi. Ndani ya eneo hilo lililo tupu, ardhi inatofautiana kutoka mashariki na magharibi.
Pwani ya Kipolandi ya Bahari ya Baltiki ni murua zaidi, lakini ina bandari asilia katika mkoa wa Gdańsk-Gdynia na Szczecin huko mashariki-magharibi ya mbali. Pwani hiyo ina upepo mzuri na maeneo kadhaa ya pwani za maziwa. Pwani za maziwa na fukwe za zamani ambazo zimekatwa kutoka baharini. Sehemu hizi pia huitwa rasi. Rasi ya Szczecin ipo upande wa mashariki mwa mpaka wa nchi ya Ujerumani. Rasi ya Vistula ipo upande wa mashariki mwa mpaka wa mji wa Kaliningrad, ambao ni katika mkoa wa Urusi.
Mto mrefu zaidi nchini Polandi ni Vistula, unaoangukia ndani ya Rasi ya Vistula na pia unakwenda moja kwa moja hadi katika Bahari ya Baltiki. Ni km 1064 kutoka chanzo hadi mdomo.
Kanda ya kaskazini-mashariki ni miti tu imejaa, inakosa watu wachache na rasilimali za kilimo na viwanda. Kanda ya kijografia ina wilaya nne za vilima vya moraine na maziwa yaliyotengenezwa na moraine. Haya yalianzishwa baada ya Pleistocene Zama za Barafu. Ziwa Masurian ni miongoni mwa maziwa manne ya wilaya yaliyochukua eneo kubwa la kaskazini-mashariki mwa Polandi.
Polandi ina maziwa kibao. Kwa Ulaya nzima, Finland peke yake ina maziwa mengi zaidi. Maziwa makubwa ni "Śniardwy" na "Mamry". Kwa kuongeza katika wilaya ya ziwa katika kaskazini, kuna idadi kubwa pia ya mlima maziwa katika milima ya Tatra.
Kusini mwa kanda ya kaskazini-mashariki mwa mikoa ya Silesia na Masovia, ambapo kuna alama za mto na mabonde ya zama za barafu. Mkoa wa Silesia una rasilimali nyingi na watu wengi. Kuna makaa ya mawe tele. Silesia ya Chini ina mgodi wa shaba mkubwa kabisa. Tambarare ya Masovian ipo kati ya Polandi. Ipo katika mabonde ya mito mikubwa mitatu: Vistula, Bug na Narew.
Ukiendelea na safari kusini ni mlima ya kanda ya Kipolandi. Milima hiyo ni pamoja na Sudetes na Milima ya Carpathi. Sehemu ndefu ya Carpathia ni milima ya Tatra ambayo imekwenda hadi kusini mwa mpaka wa nchi ya Polandi.
Mlima mrefu zaidi nchini Polandi unaitwa "Rysy" wenye m 2,503 (ft 8,210), upo Tatras.
Historia
haririWaslavi walienea kati nchi katika nusu ya pili ya karne ya 5 BK.
Ukristo wa Kikatoliki kupokewa na mfalme Mieszko I (960-992) na Wapolandi kwa jumla (966) hutazamiwa kama chanzo cha taifa lao la pekee katika jamii ya Waslavi.
Nchi ilistawi na kuenea hasa chini ya ukoo wa Jageloni (1386–1572).
Polandi-Lituanya
haririKatika miaka ya 1569–1795 Polandi iliunganishwa na Lituanya katika shirikisho la kifalme. Mfalme wa Polandi alikuwa pia mtawala wa Lithuania, na tangu mapatano ya Lublin nchi hizo mbili zilikuwa na bunge la pamoja, lakini kila sehemu iliendelea na sheria zake na jeshi la pekee. Bunge la pamoja lililokuwa hasa mkutano wa makabaila wote lilikuwa na mamlaka ya kumchagua mfalme likapata ushawishi mkubwa.
Wagombea wa ufalme waliachana na mamlaka za kifalme wakijaribu kupata kura nyingi za wabunge na hivyo nguvu ya dola ilififia.
Ugawaji wa Polandi kati ya nchi jirani
haririMwaka 1764 nchi ilianza kurudi nyuma na zile za jirani, yaani Urusi, Austria na Prussia, ziligawana kwa awamu tatu (1772, 1793, 1795) eneo lake lote. Yaani kuanzia mwaka 1772 majirani hayo matatu ya Polandi yalivamia shirikisho na kugawana maeneo yake. Kufikia mwaka 1795 maeneo yote yalikwisha kugawiwa kati ya majirani hao.
Wapolandi walijaribu mara kadhaa kujikomboa, lakini walipata uhuru kwa muda tu (1807-1815 na 1918-1939).
Baada ya vita vikuu vya pili, Polandi ikawa chini ya utawala wa Kikomunisti hadi ilipofaulu kujikomboa (1989).
Polandi imekuwa nchi mwanachama wa Umoja wa Ulaya tangu tarehe 1 Mei 2004.
Watu
haririWakazi ni 38,483,957, karibu wote wakiwa Wapolandi asili (93.52%), wakiongea Kipolandi na wakifuata Ukristo katika Kanisa Katoliki (87.5%), tena kwa bidii ya pekee.
Kati ya lugha nyingine zilizotambulika kisheria, zinaongoza Kikashubi na Kijerumani, halafu Kibelarusi na, Kiukraini. Kati ya lugha za kigeni zinaongoza Kiingereza na Kirusi.
Tazama pia
haririMarejeo
haririViungo vya nje
haririKurasa za taasisi za serikali
hariri- (Kipoland) (Kiingereza) Sejm Archived 30 Oktoba 2000 at the Wayback Machine. - Sejm - lower chamber of the Parliament
- (Kipoland) (Kiingereza) Senat Archived 15 Juni 2006 at the Wayback Machine. - Senate - upper chamber of the Parliament
- (Kipoland) (Kiingereza) Prezydent Archived 15 Juni 2006 at the Wayback Machine. - President of the Republic of Poland
- (Kipoland) (Kiingereza) KPRM Archived 5 Aprili 2005 at the Wayback Machine. - Prime Minister's Office
- (Kipoland) (Kiingereza) Sąd Najwyższy Archived 3 Aprili 2005 at the Wayback Machine. - Supreme Court
- (Kipoland) (Kiingereza) (Kifaransa) Trybunał Konstytucyjny Archived 18 Aprili 2009 at the Wayback Machine. - Constitutional Tribunal
- (Kipoland) (Kiingereza) National Bank of Poland
- (Kipoland) (Kiingereza) The Poland.pl portal
- (Kipoland) (Kiingereza) Soko la Hisa la Warshawa
- (Kipoland) (Kiingereza) GUS Archived 13 Januari 2006 at the Wayback Machine. - Central Statistical Office
- (Kipoland) (Kiingereza) Constitution of Poland
Utalii Polandi
hariri- Polish Guide of the Ministry of Foreign Affairs (poland.gov.pl) Archived 29 Oktoba 2008 at the Wayback Machine.
- Polish National Tourist Office (poland-tourism.pl, a part of pot.gov.pl) Archived 14 Juni 2006 at the Wayback Machine.
- Poland travel guide kutoka Wikisafiri
- Parks in Poland National parks, wetlands, biosphere reserves and other protected areas
Kurasa mtandaoni juu ya Polandi
hariri- Dobranoc - Free English to Polish Translation Services
- poland.gov.pl - the governmental page about Poland for international visitors Archived 29 Oktoba 2008 at the Wayback Machine.
- Centreurope.org: Poland section
- World History Database Chronology of Poland Archived 29 Agosti 2006 at the Wayback Machine.
Habari za Polandi kwa Kiingereza
hariri- Warsaw Voice, an English-language newspaper
- Warsaw Business Journal, an English-language newspaper Archived 17 Januari 2021 at the Wayback Machine.
- PolBlog - Polish News Site Archived 7 Februari 2006 at the Wayback Machine.
- - Google News listing stories about Poland
Nchi za Umoja wa Ulaya | |
---|---|
Austria | Bulgaria | Eire | Estonia | Hispania | Hungaria | Italia | Kroatia | Kupro | Latvia | Lituanya | Luxemburg | Malta | Polandi | Slovakia | Slovenia | Romania | Ubelgiji | Ucheki | Udeni | Ufaransa | Ufini | Ugiriki | Uholanzi | Ujerumani | Ureno | Uswidi |
Makala hii kuhusu maeneo ya Poland bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Polandi kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |