Marko Krisini na wenzake

Marko Krisini na wenzake[1] Stefano Pongracz[2] na Melkiori Grodziecki[3] (walifariki Kosice, leo nchini Slovakia, 7 Septemba 1619) walikuwa mapadri, wa kwanza mwanajimbo, wengine wawili wa shirika la Yesu.

Walifia imani ya Kikatoliki kwa amri ya mfalme Mprotestanti Gabor Bethlen.

Wanaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama watakatifu wafiadini. Kwanza walitangazwa na Papa Pius X kuwa wenye heri tarehe 15 Januari 1905, halafu watakatifu na Papa Yohane Paulo II tarehe 2 Julai 1995.

Sikukuu yao huadhimishwa tarehe ya kifodini chao[4].

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.