Marselo wa Tanja (au Marselo akida; alifariki huko 30 Oktoba[1] 298) alikuwa askari huko Tanja (leo nchini Moroko) aliyefia imani yake kwa kukatwa kichwa katika dhuluma ya kaisari Diocletian kwa sababu wakati watu wote walikuwa wakitoa sadaka kwa miungu kwa sikukuu ya kaisari, yeye alitupilia mbali mkanda wa jeshi, silaha na uhai wenyewe mbele ya bendera, akijitangaza Mkristo na kwamba hawezi tena kutekeleza sawasawa kiapo chake jeshini, bali kumtii Yesu tu[2].

Picha takatifu ya Marselo na Kasiani wa Tanja katika kanisa la Kiorthodoksi la Rabat, Moroko.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 30 Oktoba[3].

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri
  1. Geoffrey Ernest Maurice de Sainte-Croix, Christian Persecution, Martyrdom, and Orthodoxy, Oxford University Press, 2006, p. 172:"we must admit that we know nothing of the date or the circumstances of his execution"
  2. https://www.santiebeati.it/dettaglio/75700
  3. Martyrologium Romanum

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.