Mary Calderone

Daktari wa Marekani (1904-1998)

Mary Steichen Calderone( Julai 190424 Oktoba 1998) alikuwa daktari na mtetezi wa afya ya umma na utoaji elimu ya [ngono]]. Kazi yake kuu ilikuwa kubatilisha sera ya chama cha madaktari cha nchini Marekani dhidi ya usambazaji wa taarifa za udhibiti wa uzazi kwa wagonjwa.

Mary Steichen Calderone

Calderone aliwahi kuwa raisi na mwanzilishi mwenza wa baraza la habari za jinsia na elimu la Marekani Sex Information and Education Council of the United States (SIECUS) kuanzia mwaka 1954 hadi 1982. Pia alikuwa mkurugenzi wa matibabu wa uzazi wa mpango. Aliandika machapisho mengi yanayotetea mazungumzo ya wazi na upatikanaji wa habari katika umri wote. Kazi yake kubwa ya kueneza elimu ya kujamiiana mara nyingi imelinganishwa na kampeni ya Margaret Sanger ya udhibiti wa uzazi.

Marejeo hariri

  Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mary Calderone kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.