Masifu ya jioni

(Elekezwa kutoka Masifu ya Jioni)

Masifu ya jioni ni kipindi muhimu zaidi cha Sala ya Kanisa katika madhehebu mbalimbali ya Ukristo.[1][2]

Wabenedikto wakiimba Masifu ya jioni kwenye Jumamosi kuu.
Ubani ukifukizwa wakati wa kuimba Magnificat kwenye Majilio.
Padri na shemasi wa Kiorthodoksi wakiingia patakatifu wakiwa na chetezo.

Ni sala rasmi inayofanyika wakati wa jua kuelekea kutua ili kumshukuru Mungu kwa siku inayokaribia kwisha.[3]

Katika utaratibu wa Kanisa la Roma, unaofuatwa na majimbo karibu yote ya Kanisa Katoliki la Kilatini, sehemu kuu za sala hiyo, kati ya utangulizi na baraka ya mwisho, ni utenzi, zaburi mbili (au moja ndefu iliyogawiwa pande mbili), wimbo kutoka Nyaraka za Mitume au kitabu cha Ufunuo, somo fupi au refu kutoka Agano Jipya, kiitikizano, wimbo wa Bikira Maria, maombezi, Baba Yetu na sala ya kumalizia.

Kati ya sehemu hizo, kilele ni maneno ya Injili (wimbo wa Bikira Maria na Baba Yetu).

Tanbihi hariri

  1. Home - Christ Church Cathedral Vancouver. Cathedral.vancouver.bc.ca (2015-05-15). Jalada kutoka ya awali juu ya 2009-02-14. Iliwekwa mnamo 2015-05-22.
  2. Keith Danby. Welcome to Christ Church Deer Park - There's Life Here!. Christchurchdeerpark.org. Iliwekwa mnamo 2015-05-22.
  3. name=usccb>Vespers. Usccb.org (2013-04-16). Iliwekwa mnamo 2015-05-22.

Viungo vya nje hariri

 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Masifu ya jioni kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.