Masima, Donatila na Sekunda
Masima, Donatila na Sekunda (walifariki 303) walikuwa mabikira Wakristo wa Taburba (leo nchini Tunisia) waliouawa kwa ajili ya imani yao wakati wa dhuluma ya kaisari Diokletian.
Wawili wa kwanza walikataa bila woga kutekeleza amri yake ya kutoa sadaka kwa miungu na kwa hukumu ya liwali Anulino walitupwa kwanza kwa wanyamapori ili waliwe nao, halafu wakakatwa kichwa pamoja na mtoto Sekunda[1].
Tangu kale wanaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama watakatifu.
Tazama pia
haririTanbihi
haririMakala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |