Matendo ya Perpetua na Felista

"Matendo ya Perpetua na Felista" (kwa Kilatini: Acta Perpetuae et Felicitatis) ni maandishi ya pekee kwa sababu yanatunza kumbukumbu za wafiadini hao wa Ukristo gerezani na wataalamu huamini ya kwamba zimeandikwa na Perpetua Mtakatifu mwenyewe (sura III-X). Kama hii ni kweli, ni maandiko ya kale kabisa ya mwanamke Mkristo katika historia iliyotunzwa.

Kifodini cha Mt. Perpetua, Felista na wenzake katika vioo vya kanisa la Bikira Maria huko Vierzon (karne ya XIX).

Kitabu kiliandikwa muda mfupi tu baada ya akina mama hao vijana kuuawa tarehe 7 Machi 203 mjini Karthago wakati wa dhuluma dhidi ya Wakristo chini ya serikali ya Kaisari Septimius Severus (193-211).

Pamoja na wanaume 4 walihukumiwa adhabu ya kifo katika uwanja wa michezo mbele ya watu wengi. Hukumu ilitekelezwa kwa njia ya wanyamapori.

Jinsi maandishi hayo yalivyoheshimika inadhihirika katika maonyo aliyotoa Agostino wa Hippo (karne mbili baadaye) ya kwamba yasiheshimiwe sawa na Biblia.

Pamoja na hayo, mvuto wa habari hizo haujaisha hata leo.

Tazama pia hariri

Filamu hariri

  • Perpetua: Early Church Martyr (2009) - documentary.
  • Torchlighters: The Perpetua Story (2009) - animated DVD for children ages 8–12.

Viungo vya nje hariri

  Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Matendo ya Perpetua na Felista kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.