Perpetua Mtakatifu

Perpetua (181 - 7 Machi 203) alikuwa mama kijana mjini Karthago (leo nchini Tunisia) wakati wa Dola la Roma alipouawa kama shahidi wa imani ya Kikristo.

Picha ya Perpetua (mnamo 1280) katika kanisa la Porec - Kroatia.
Kifodini cha Mt. Perpetua na wenzake katika uwanja wa michezo, kinavyoonyeshwa katika vioo vya kanisa la Bikira Maria huko Vierzon, karne XIX.
Sanduku la Mt. Perpetua katika kanisa hilo la Vierzon.

Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki, Waorthodoksi, Waanglikana, Walutheri na wengineo kati ya watakatifu wafiadini na sikukuu yake ni tarehe 7 Machi[1].

Perpetua anakumbukwa pamoja na mtumwa na rafiki yake Felista na wavulana wanne ambao aliuawa pamoja nao: Saturus, Revokatus, Saturninus na Sekondinus.

Maisha hariri

Perpetua alikuwa binti wa familia tajiri.

Kwenye umri wa miaka 21 aliolewa akapata mtoto. Wakati ule alijiandaa kubatizwa pamoja na watumwa wake Felista na Revocatus na kijana mwingine aliyeitwa Saturninus. Walikamatwa pamoja na mwalimu wao Saturus na wakatekumeni wengine wa kike katika wimbi la dhuluma dhidi ya Wakristo chini ya serikali ya Kaisari Septimius Severus (193-211).

Kwanza Perpetua alifungwa ndani na kupewa nafasi ya kuachana na imani yake. Alipokataa alihukumiwa adhabu ya kifo pamoja na wenzake. Gerezani walipokea ubatizo.

Perpetua alibembelezwa sana na babaye Mpagani aachane na Ukristo na kuokoa uhai wake, lakini alikataa.

Pamoja na wenzake aliuawa katika uwanja wa michezo mbele ya watu wengi. Hukumu ilitekelezwa kwa njia ya wanyamapori. Yeye na Felista walitokea gerezani kuingia uwanjani wakiwa wafurahivu kama kwenda mbinguni.

Heshima baada ya kifo hariri

Heshima iliyotolewa mara kwa wafiadini hao ilienea haraka katika Kanisa lote.

Masalia ya Perpetua yalihamishwa mara kadhaa kutoka na matatizo ya kihistoria. Hatimaye yamehifadhiwa huko Vierzon (Ufaransa).

Matendo ya Perpetua na Felista hariri

"Matendo ya Perpetua na Felista" ni maandishi ya pekee kwa sababu kuna kumbukumbu ambazo zinasimulia habari zake gerezani na wataalamu huamini ya kwamba zimeandikwa na Perpetua mwenyewe (sura III-X). Kama hii ni kweli, ni maandiko ya kale kabisa ya mwanamke Mkristo katika historia iliyotunzwa.

Filamu hariri

  • Perpetua: Early Church Martyr (2009) - documentary.
  • Torchlighters: The Perpetua Story (2009) - animated DVD for children ages 8–12.

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

Viungo vya nje hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.