Msongozi
Msongozi ni kata ya Wilaya ya Mvomero katika Mkoa wa Morogoro, Tanzania.
Kata ya Msongozi ina vijiji vitatu, navyo ni Msongozi, Mkata, na Mtipule. Kijiji cha Msongozi ndicho kijiji kikubwa zaidi. Kijiji hicho kina vitongoji 10, navyo ni Mbogeni, Pasua, Kwata Stoo, Gwata Msikitini, Mwenyemla, Gole (Majengo), Kitanga, Mishieni (Mission), Lusanga, na Yowe.
Makao makuu ya kata yapo Gwata Stoo, na ndicho kitongoji mjini zaidi kwa kata nzima kikifuatiwa na Gwata Msikitini. Lusanga na Yowe ni maarufu kwa mazao ya chakula na ya biashara kama vile mahindi, maharage, mbaazi, ndizi na mihogo. Gwata Stoo na Msikitini ni maarufu zaidi kwa maduka na kilimo cha biashara cha nyanya. Mishieni ni maarufu kwa kuwa ni gulio kuu la bidhaa za kilimo hasa kutoka Lusanga na Yowe.
Kijiji cha Mkata kinapakana na wilaya ya Kilosa, na ni maarufu kwa uvuvi wa samaki na kilimo cha mpunga.
Wakazi
haririKatika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 5,155 [1].
Wakazi wa asili wa kata hii ni Waluguru. Wageni kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania wamehamia kwenye kata hii, wakiwemo Wahehe na Wamasai. Hao wa mwisho ni wafugaji waliofika hapa kwa kuhamahama lakini kutokana na hali bora ya malisho kwa mifugo yao wamekuwa na makazi ya kudumu hapa.
Marejeo
haririKata za Wilaya ya Mvomero - Mkoa wa Morogoro - Tanzania | ||
---|---|---|
Bunduki | Dakawa | Diongoya | Doma | Hembeti | Homboza | Kanga | Kibati | Kikeo | Kinda | Kweuma | Langali | Luale | Lubungo | Mangae | Maskati | Melela | Mgeta | Mhonda | Mkindo | Mlali | Msongozi | Mtibwa | Mvomero | Mziha | Mzumbe | Nyandira | Pemba | Sungaji | Tchenzema |
Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Morogoro bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Msongozi kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. Tafadhali usiingize majina ya maafisa na viongozi wa sasa maana wanabadilika haraka mno. |