Mpwa ni jina ambalo mwanamume anamuita mtoto (wa kiume au wa kike) wa dada yake. Upande wa pili, mpwa anamuita mwanamume huyo "mjomba".

Ukilinganisha na lugha za Ulaya, zile za Kibantu zinazingatia zaidi umri na hasa jinsia za wazazi na ndugu zao. Hivyo, kwa Kiingereza "nephew" linaweza kumaanisha "mpwa" lakini pia "mtoto" (ikiwa anayesema ni wa jinsia ileile ya mzazi).

Tena anayeitwa kwa Kiingereza "uncle" anaweza akaitwa katika Kiswahili "mjomba", "baba mkubwa" (kama ni kaka wa baba) au "baba mdogo" (kama ni mdogo wa baba). Vilevile neno "aunt" linaweza kumaanisha "shangazi" (dada wa baba), "mama mkubwa" (kama ni mkubwa wa mama) au "mama mdogo" (kama ni mdogo wa mama).

Wajibu na haki kati ya mpwa na mjomba wake vinategemea utamaduni wa mahali. Katika baadhi ya makabila, kama yale yanayotia maanani ukoo wa mama kuliko ule wa baba, mjomba ni muhimu kuliko baba mzazi.

Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mpwa kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.