Mkoa wa Kaskazini-Mashariki (Kenya)

Mikoa ya Kenya
Mkoa wa Kaskazini-Mashariki
North Eastern Province
Mahali pa Mkoa wa Kati
Makao Makuu Garissa
’‘‘Mji Mkubwa’’’ Garissa
Eneo

- Jumla
Nafasi ya 3 kati ya mikoa ya Kenya
126,186 km²
Wakazi
(kadirio)

 - Jumla (2007)  - Msongamano wa watu / km²
Nafasi ya 8 kati ya mikoa ya Kenya
459,000
4 /km²
Lugha mkoani Kisomali
Kioromo

Kaskazini-Mashariki ulikuwa mmoja kati ya mikoa 9 ya Kenya. Eneo lake lilikuwa km² 127 000 [1] Ilihifadhiwa 29 Novemba 2006 kwenye Wayback Machine. na wakazi 962,143 (sensa ya 1999).

Wakati wa ukoloni eneo hilo liliitwa "Northern Frontier District" (Eneo la mpakani wa kaskazini) likitawaliwa pekee na sehemu kubwa ya Kenya.

Wakazi walio wengi ni Wasomalia kwa lugha na utamaduni; kuwepo kwao ndani ya Kenya badala ya Somalia ni urithi wa mipaka ya kikoloni. Wengine ni Waborana, Warendille na Waturkana.

Kuna pia makambi makubwa ya wakimbizi Wasomalia, hasa karibu na Daadab.

Hali ya hewa

hariri

Eneo hili ni kavu sana. Mbali na bonde la mto Tana na maeneo mengine madogo, mkoa haufai kwa kilimo. Wakazi walio wengi hujipatia riziki kutokana na ufugaji.

Utawala

hariri

Mkoa wa Kaskazini-Mashariki ulikuwa na wilaya nne: