Mkunga
Mkunga-chui mkubwa (Gymnothorax javanicus)
Mkunga-chui mkubwa (Gymnothorax javanicus)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Actinopterygii
Oda: Anguilliformes
L.S. Berg, 1943
Ngazi za chini

Nusuoda 8:

Mikunga ni samaki wa baharini na/au maji baridi katika oda Anguilliformes walio na umbo la nyoka.

Hufanyiwa maendeleo makubwa kutoka hatua ya mapema ya lava hadi hatua ya mwisho ya waliokomaa, na wengi ni samaki mbuai.

Ufafanuzi

hariri

Mikunga ni samaki waliorefuka wenye urefu wa sm 5 katika Mkunga Taya-moja (Monognathus ahlstromi) hadi m 4 katika Mkunga-chui Mkubwa Mwembamba. Waliokomaa wana uzito kutoka g 30 hadi zaidi ya kg 25.

Hawana mapezi ya tumbo, na spishi nyingi hazina mapezi ya mbavu pia. Mapezi ya mgongo na ya mkundu yameungana na pezi la mkia na pamoja yanaunda utepe mmoja unaoenda kiasi cha urefu wa mnyama. Mikunga huogelea kwa kuzalisha mawimbi ya mwili ambayo husafiri urefu wa mwili wao. Wanaweza kuogelea kisengesenge kwa njia ya kupindua mwelekeo wa wimbi.

Mikunga wengi sana huishi katika maji kame ya bahari na huingia kwenye mchanga, matope au katikati ya miamba. Takriban spishi zote za mikunga hukiakia usiku na kwa hivyo huonekana kwa nadra. Wakati mwingine huonekana wakiishi pamoja katika mashimo yaitwayo "mashimo ya mikunga". Spishi fulani za mikunga huishi katika maji ya kina kirefu zaidi ya matako ya mabara na ya miteremko yao yenye kina cha hadi m 4,000. Wanajenasi wa Anguilla hukaa maji baridi kwa muda mrefu, lakini hata hawa wanarudi baharini ili kuzaliana.

Mzunguko wa maisha

hariri

Mikunga huanza maisha yao kama lava angavu inayoitwa leptocephali. Lava wa mikunga huelea kwenye maji yaliyo juu ya bahari, wakijilisha theluji ya bahari, chembe ndogo zinazoelea ndani ya maji. Halafu hubadilika umbo kuwa mikunga-kioo na kisha kuwa mikunga wachanga kabla ya hatimaye kutafuta makazi yao ya kitoto na yale ya waliokomaa. Mikunga wengi wanabakia baharini muda wa maisha yao yote, lakini mikunga wachanga wa maji baridi wa familia Anguillidae husafiri katika mito dhidi ya mkondo na wanalazimika kupanda juu ya vikwazo kama vile vizingiti, kuta za maboma ya maji na maporomoko ya maji ya asili.

 
Mzunguko wa maisha wa mkunga wa kawaida

Mwainisho

hariri

Mwainisho huu unafuatia "FishBase" ukigawanya mikunga katika familia 20. Familia za ziada zilizojumuishwa katika miainisho mingine (hasa ITIS na Systema Naturae 2000 zinajulikana chini ya familia iliyo ni kisawe chake katika mfumo wa FishBase.

Kutambua jadi ya spishi za maji baridi ilikuwa tatizo. Uchunguzi wa kijenomu unaonyesha kuwa ni kundi la nasaba moja lililotoka baina ya mikunga wa bahari.

Spishi zilizochaguliwa za Afrika ya Mashariki

hariri

Marejeo

hariri
  • Rashid Anam & Edoardo Mostarda (2012) Field identification guide for the living marine resources of Kenya. FAO, Rome.
  • Gabriella Bianchi (1985) Field guide to the commercial marine brackish-water species of Tanzania. FAO, Rome.

Viungo vya nje

hariri