Anguilla ni kisiwa cha Antili Ndogo katika Karibi na pamoja na visiwa vidogo visivyo na wakazi ni eneo la ng'ambo la Uingereza.

Anguilla
Ramani ya Anguilla
Mahali pa Anguilla

Kisiwa kikubwa cha Anguilla kina urefu wa 25 km na upana wa 3 km; eneo lake ni 103 km² na idadi ya wakazi mnamo watu 13,500. Kipo upande wa mashariki ya Puerto Rico na upande wa kaskazini ya Saint-Martin.

Anguilla iliwahi kuwa sehemu ya Saint Kitts na Nevis ikajitenga 1980 na kubaki sehemu ya Uingereza wakati visiwa vingine kupata uhuru.

Jina ni neno la Kihispania kwa samaki ya mkunga kutokana na umbo lake kuwa ndefu na nyembamba.

Uchumi wa kisiwa hutegemea hasa uvuwi na utalii.

Watu wa Angulilla wana asili ya watumwa kutoka Afrika. Lugha ya ni Kiingereza.

Caribe-geográfico.svg Makala hii kuhusu maeneo ya Bahari ya Karibi bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Anguilla kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu: