Etna
(Elekezwa kutoka Mlima Etna)
Kwa maana nyingine, tazama Etna (maana).
Etna (kutoka Kilatini: Aetna; kwa Kiitalia pia Mongibello; kwa Kisisili Mungibeddu au â Muntagna) ni volkeno hai wa Sicilia mashariki (Italia visiwani) kati ya miji ya Catania na Messina. Ndiyo ndefu kuliko zote za Ulaya[1]: kwa sasa imefikia mita 3357 juu ya usawa wa bahari.[2]
Etna inaenea katika kilometa mraba 1190 ukiwa na duara ya km 140 miguuni pake. [3]
Etna inakadiriwa kuwa na miaka 350,000 - 500,000 na ni kati ya volkeno hai zaidi duniani, kwa kuwa haitulii karibu kamwe, lakini kwa namna yake si hatari. Lava yake inageuka baada ya miaka kadhaa kuwa nzuri sana kwa kilimo.
Mnamo Juni 2013 iliingizwa na UNESCO katika orodha ya urithi wa dunia.[4]
Tanbihi
hariri- ↑ http://www.volcano.group.cam.ac.uk/volcanoes/etna/
- ↑ https://www.ct.ingv.it/index.php/formazione-e-divulgazione/news/303-l-etna-si-supera-nuovo-record-di-altezza-a-3357-metri
- ↑ "Italy volcanoes and Volcanics". USGS.
- ↑ Mount Etna Becomes a World Heritage Site, Italy Magazine, 4 Mei 2013
{{citation}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
Marejeo
hariri- "Etna". Global Volcanism Program, Smithsonian Institution. http://www.volcano.si.edu/world/volcano.cfm?vnum=0101-06=. Retrieved 2008-12-25.
- Chester, D. K.; Duncan, A. M.; Guest, J. E.; Kilburn, C. R. J. (1985). Mount Etna: The Anatomy of a Volcano. Chapman and Hall. ku. 412 pp. ISBN 0-8047-1308-1.
Viungo vya nje
hariri- Mount Etna Live Webcams Ilihifadhiwa 26 Januari 2017 kwenye Wayback Machine.
- Mount Etna Face Nord Live Webcams
- Mount Etna Regional Park
Makala hii kuhusu maeneo ya Italia bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Etna kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |