Ezekiel Kemboi
Ezekiel Kemboi Cheboi (alizaliwa 25 Mei 1982) ni mwanamichezo wa Kenya, mshindi wa mbio ya mita 3000 ya kuruka viunzi katika Olimpiki ya 2004 na Mbio ya Dunia ya Mabingwa 2009.
Alizaliwa Matira, karibu na Kapsowar katika Wilaya ya Marakwet. Kemboi alimaliza masomo ya shule ya upili katika Shule ya sekondari ya wavulana ya Kapsowar katika mwaka 1999. Hakuanza mazoezi ya riadha hadi baada ya kutoka shule. Paul Ereng aliona talanta yake ndipo baadaye akashinda Mbio ya Vijana ya Afrika hapo waka wa 2001 ingawa alianguka chini.
Katika mwaka wa 2002,Ezekiel Kemboi alimaliza katika nafasi ya pili katika Michezo ya Jumuiya ya Madola nyuma ya mwenzake kutoka Kenya,Stephen Cherono. Kemboi mwaka huo alikuwa # 4 hapo awali katika Mbio ya Mabingwa wa Afrika katika Riadha, lakini baadaye akatuzwa na medali ya shaba baada ya mshindi kutoka Morocco Brahim Boulami alinyang'anywa medali kwa kutumia dawa za kumpa nguvu.
Wakati wa Mbio ya Mabingwa wa Dunia ya 2003, Kemboi alikuwa katika shindano kali na aliyekuwa mwenzake Saif Saeeed Shaheen (aliyekuwa Stephen Cherono) aliyewakilisha nchi yake mpya,Qatar.Shaheen alimwacha Kemboi aliyekuwa amechoka na kushinda mbio hiyo kwa muda chini ya sekunde tu. Kemboi alishinda medali ya dhahabu katika Michezo ya Afrika ya 2003.
Katika kutokuwepo kwa Shaheen - Kamati ya Olimpiki ya Kenya ilikataa kumwondolea sheria inayokataza mwanariadha kushiriki katika Olimpiki kama alibadili uraia wake kama amekuwa mwanariadha maarufu.Hivyo basi, Kemboi ndiye aliyekuwa anayeonekana kushinda mbio hiyo huko Athens. Mbio hiyo ilienda kama ilivyofaa,Wakenya watatu :Kemboi, Brimin Kipruto na Paul Kipsiele Koech akiendesha mbio hizo kutoka raundi ya pili na kuwaacha wengine kwa mbali na Kemboi akashinda medali ya dhahabu kwa sekunde 0.3 mbele ya Kipruto.
Katika mwezi wa Agosti 2005,yeye alishinda medali ya fedha katika Mbio yaMabingwa wa Dunia katika Riadha katika mwaka wa 2005 , na hapo Machi 2006 yeye alishinda mbio hiyo ya MIchezo ya Jumuiya ya Madola ya 2006. Yeye alimaliza akiwa wa pili katika mbio ya Mabingwa wa Afrika wa 2006 lakini akatolewa kwa kuruka viunzi vibaya.
Meneja wa Kemboi ni Enrico Dionisi. Tangu mwaka wa 2002 amemiliki [16] shamba karibu na Moi's Bridge,Wilaya ya Trans-Nzoia. [17] Yeye ni alioa na Jane Kemboi na ana wana wawili. Tangu mwaka wa 2009,amekuwa akifanywa mazoezi na Moses Kiptanui ambaye ni jirani yake.
Tuzo
haririMwaka | Shindano | Pahala pa kushindana | Tokeo | Maelezo ya ziada |
---|---|---|---|---|
2001 | Mbio ya Vijana ya Mabingwa | Réduit, Mauritius | 1 | 3000 m kuruka viunzi |
2002 | Michezo ya Jumuiya ya Madola | Manchester, Uingereza | 2 | 3000 m kuruka viunzi |
Michezo ya Mabingwa wa Afrika wa Riadha | Radès, Tunisia | 4 | 3000 m kuruka viunzi | |
2003 | Mbio za Afrika za 2003 | Abuja, Nigeria | 1 | 3000m kuruka viunzi |
Mbio ya Mabingwa katika Riadha ya 2003 | Paris, Ufaransa | 2 | 3000 m kuruka viunzi | |
Mbio za IAAF za 2003 | Monte Carlo, Monaco | 3 | 3000 m kuruka viunzi | |
2004 | Olimpiki ya 2004 | Athens, Ugiriki | 1 | 3000m kuruka viunzi |
Mbio za Fainali za IAAF za 2004 | Monte Carlo, Monaco | 2 | 3000 m kuruka viunzi | |
2005 | Mbio ya Mabingwa ya 2005 | Helsinki, Finland | 2 | 3000m kuruka viunzi |
Mbio za Fainali za IAAF | Monte Carlo, Monaco | 2 | 3000 m kuruka viunzi | |
2006 | Michezo ya Jumuiya ya Madola | Melbourne, Australia | 1 | 3000 m kuruka viunzi |
Mbio za Fainali za IAAF za 2006 | Stuttgart, Ujerumani | 5 | 3000 m kuruka viunzi | |
2007 | Mbio za Afrika za 2007 | Algiers, Algeria | 2 | 3000 m kuruka viunzi |
Mbio ya Mabingwa wa Dunia | Osaka, Ujapani | 2 | 3000m kuruka viunzi | |
2008 | Olimpiki ya 2008 | Beijing, Uchina | 7 | 3000m kuruka viunzi |
Mbio za Fainali za IAAF | Stuttgart, Ujerumani | 2 | 3000 m kuruka viunzi | |
2009 | Mbio za Mabingwa wa Dunia za 2009 | Berlin, Ujerumani | 1 | 3000m kuruka viunzi |
Mbio za Fainali za IAAF | Thessaloniki, Ugiriki | 1 | 3000 m kuruka viunzi |
References
hariri- ^ a b c IAAF, 24 Agosti 2004: Ezekiel Kemboi (KEN) Ilihifadhiwa 4 Agosti 2012 kwenye Wayback Machine.
- ^ The Standard, 21 Agosti 2009: Kemboi ashukuru familia baada ya ushindi katika mji wa Berlin Ilihifadhiwa 29 Oktoba 2009 kwenye Wayback Machine.
Viungo vya nje
hariri- Kemboi kwenye IAAF Ilihifadhiwa 18 Oktoba 2012 kwenye Wayback Machine.
- IAAF, 24 Agosti 2004: Ezekiel Kemboi (KEN) Ilihifadhiwa 4 Agosti 2012 kwenye Wayback Machine.