Mrisho Ngassa

Mwanasoka wa Tanzania

Mrisho Ngassa (alizaliwa tarehe 5 Mei 1989) ni mchezaji wa mpira wa miguu kutoka Tanzania ambaye aliichezea klabu ya Ndanda FC na pia yanga African pia aliichezea timu ya taifa ya Tanzania.

Mrisho Halfani Ngassa
Maelezo binafsi
Jina kamili Mrisho Halfani Fyade Ngassa
Tarehe ya kuzaliwa 5 Mei 1989 (1989-05-05) (umri 35)
Mahala pa kuzaliwa    Mwanza, Tanzania
Urefu 1.64
Nafasi anayochezea Mrengo wa kushoto
Maelezo ya klabu
Klabu ya sasa Ndanda FC
Namba 7
Klabu za vijana
Young Africans FC
Klabu za ukubwani
Miaka Klabu
Kagera Sugar 2004-2005

Young Africans2005-2011

Azam FC 2011-2012

Simba2012-2013 mkopo

Young Africans 2013-2015

Free state stars 2015-2016

Mbeya City 2016-2017

Ndanda FC 2017-2018

Yanga Sc 2018-2020

Timu ya taifa
Tanzania

* Magoli alioshinda

Majaribio West Ham United

hariri

Mwezi wa Aprili 2009, Ngassa kutokana na uchezaji wake mzuri alialikwa na klabu ya Uingereza iitwayo West Ham United kwa majaribio ya wiki mbili ili waweze kumnunua, majaribio yalipoisha West Ham ilizungumzwa kuwa ni mchezaji mzuri ila anahitaji baadhi ya vitu fulani navyo ni vya kiufundi katika mambo ya mpira hata hivyo inazungumzwa kuna baadhi ya klabu barani Ulaya zinapendelea kumchukua.

Timu ya Taifa ya Tanzania

hariri

Katika mashindano ya Cecafa 2009 yaliyofanyika Kenya alijinyakulia ubingwa wa mfungaji bora katika mashindano hayo kwa kuweza kufunga mabao ma 5 katika shindano hilo lakini timu yake ya taifa ya Tanzania ilichukua nafasi ya Nne katika mashindano hayo.

Ngassa ni kijana ambae anaangaliwa kua atakua na mustakabali mzuri wa nchi yake na Afrika pia. 21 Mei 2010 alijiunga na Azam FC baada ya majaribio.

Mnamo Julai 2011 alijaribiwa na Seattle Sounders akaja kama mchezaji dhidi ya Manchester United katika mechi ya kirafiki. Baada ya muda alijiunga na kikosi cha Simba S.C.

Viungo vya nje

hariri