Ngarara
Ngarara mamba (Tylosurus crocodilus)
Ngarara mamba (Tylosurus crocodilus)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Actinopterygii (Samaki walio na mapezi yenye tindi)
Oda: Beloniformes (Samaki kama ngarara)
Familia: Belonidae (Samaki walio na mnasaba na ngarara)
Bonaparte, 1832
Ngazi za chini

Jenasi 10 na spishi 35, 9 katika Afrika:

Ngarara, ngarengare, watumbuudau, watumbuu, mgendi, mgezi au mikule ni samaki za baharini na maji baridi wa familia Belonidae katika oda Beloniformes.

Maelezo

hariri

Ngarara ni wembamba na huwa na urefu wa sm 3 hadi 95. Wana pezimgongo moja lililopo nyuma sana kwenye mwili, takriban mkabala na pezimkundu. Sifa yao bainifu zaidi ni domo lao refu na jembamba, ambalo huwa na meno mengi makali. Katika spishi nyingi taya la juu linafikia urefu wake kamili wakikomaa, hivyo wana wanaonekana kama chuchunge wenye taya la chini lililorefuka lakini lile la juu dogo zaidi sana. Wakati wa hatua hii ya maisha yao, hula planktoni na kubadilisha mpaka samaki baada ya kukomaa kikamilifu kwa domo. Ngarara huzaana kwa kujamiiana na kutaga mayai. Kwa kawaida dume hupanda jike juu ya mawimbi wakati wakijamiiana.

Ekolojia

hariri

Ngarara wote hujilisha hasa kwa samaki wadogo, ambao wanawakamata kwa msogeo kasi kuelekea juu wa kichwa chao. Aidha, spishi fulani hukamata pia krili, gegereka wanaoogelea na sefalopodi wadogo. Spishi za maji ya chumvi ni mbuai pia na angalau spishi ya Uhindi hujilisha kwa gegereka wakubwa tu.

Ngarara wapo kawaida katika nusutropiki, lakini baadhi hukaa maji ya wastani pia, hasa wakati wa baridi. Ngarara wa Ulaya, spishi ya kawaida ya Bahari ya Atlantiki ya Kaskazini, huogelea mara nyingi kwa makundi pamoja na jodari. Hupatikana katika makazi ya maji kame ya bahari au karibu na uso wa bahari ya wazi. Jenasi kadhaa zinajumuiya spishi zilizopatikana katika mazingira ya maji ya bahari, maji ya chumvi kidogo na maji baridi (k.m. Strongylura), lakini jenasi chache zinatokea kwenye mito na vijito ya maji baridi (k.m. Belonion, Potamorrhaphis na Xenentodon).

Hatari kwa binadamu

hariri

Ngarara, kama Beloniformes wote, wanaweza kufanya miruko mifupi nje ya maji kwa mbio za hadi km 60 kwa saa. Kwa sababu ngarara huogelea karibu na uso wa maji, mara nyingi huruka kupitia sitaha ya mashua madogo badala ya kuzunguka. Utenzi huu wa kuruka unaongezwa sana na mwanga wa bandia usiku. Wavuvi wa usiku na wazamaji katika maeneo ya Bahari ya Pasifiki wamekuwa "wakishambuliwa" na makundi ya ngarara waliochochewa ghafla wakiruka juu ya maji kuelekea chanzo cha mwanga kwa kasi kubwa. Madomo yao makali yanaweza kusababisha majeraha ya kutoboa mbali yakikonyoleka mara nyingi ndani ya mwathirika. Kwa jamii nyingi za jadi za Visiwa vya Pasifiki, ambazo huvua samaki juu ya miamba ya marijani kutoka kwenye mashua madogo, ngarara huwa hatari ya kuumia zaidi kuliko papa.

Spishi za Afrika

hariri

Marejeo

hariri
  • Rashid Anam & Edoardo Mostarda (2012) Field identification guide for the living marine resources of Kenya. FAO, Rome.
  • Gabriella Bianchi (1985) Field guide to the commercial marine brackish-water species of Tanzania. FAO, Rome.

Viungo vya nje

hariri