Nikanori mwinjilisti

Nikanori mwinjilisti (alifariki Kupro, 76) ni Myahudi wa karne ya 1 anayejulikana hasa kutokana na Matendo ya Mitume.

Mchoro wa ukutani wa Fra Angelico, ukionyesha Mtume Petro akiweka wakfu wainjilisti saba wa kwanza.

Anaheshimiwa na madhehebu mbalimbali ya Ukristo kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa na Kanisa Katoliki na Anglikana tarehe 28 Julai[1][2].

Katika Biblia hariri

Alikuwa mmojawapo kati ya wanaume saba wa lugha ya Kigiriki katika Kanisa mama la Yerusalemu waliochaguliwa kushughulikia mafukara kwa niaba ya Mitume wa Yesu (Mdo 6).

Katika mapokeo hariri

Mapokeo ya baadaye yanasimulia kwamba alikwenda Kupro na huko alifia dini yake.

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  1. "Martyrologium Romanum", Typis Vaticanis, Editio Altera, 2004
  2. Calendar of saints (Episcopal Church in the United States of America)

Viungo vya nje hariri

 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.