Onesimo (kwa Kigiriki Ὀνήσιμος, Onēsimos, yaani "Wa kufaa"; labda alifia dini Roma, Italia, mwaka 68 hivi),[1] alikuwa mtumwa wa Filemoni, Mkristo tajiri wa Kolosai, leo nchini Uturuki.

Picha ya kifodini cha Onesimo, kutoka Menologion ya Basili II (1000 BK hivi).

Anaheshimiwa na madhehebu mbalimbali ya Ukristo kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 15[2] au 16 au 28 Februari, au tarehe 22 Novemba.

Katika Biblia Edit

Jina "Onesimo" linatajwa katika Nyaraka mbili za Mtume Paulo: Waraka kwa Wakolosai 4:9[3] na Waraka kwa Filemoni ambao uliandikwa wote ili kumtetea.

Ni kwamba Onesimo alikuwa amemkimbia Filemoni na labda alimuibia pia. Lakini baadaye alikutana na Mtume Paulo (ama Roma ama Kaisarea)[4][5] akaongokea Ukristo. Paulo, aliyekuwa amekwisha kumuongoa Filemoni pia, aliamua kuwapatanisha kwa barua iliyomo sasa katika Agano Jipya.[6]).

Tazama pia Edit

Tanbihi Edit

  1. Onesimus. Ecumenic Patriarchate of Constantinople. Jalada kutoka ya awali juu ya 2016-03-03. Iliwekwa mnamo Apr 2, 2011.
  2. Martyrologium Romanum
  3. Christian Bible: Colossians 4:9
  4. 'The Letter to Philemon', Joseph A. Fitzmyer S.J., paragraph 5, pages 869-870 The New Jerome Biblical Commentary, 1989, Geoffrey Chapman
  5. Saint Onesimus at SQPN website. Jalada kutoka ya awali juu ya 2006-12-24. Iliwekwa mnamo 2016-01-23.
  6. Christian Bible: Philemon verses 19-16

Viungo vya nje Edit

  Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Onesimo kama habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.